TOSCI Yapongezwa Kwa Ukarabati wa Maabara ya Taifa ya Mbegu

0


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli ameipongeza Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kwa ujenzi wa jengo na ukarabati wa maabara ya Taifa ya Mbegu kwa gharama ya Shilingi Bilioni 1.8 iliyopo mkoani Morogoro na kuitaka Taasisi hiyo kutoa vibali kwa mbegu zilizothibitishwa ndani ya siku 7 hadi 14 kutokana na aina ya mbegu.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha tija inapatikana na tija hiyo huanzia kwenye mbegu bora,” ameeleza Katibu Mweli tarehe 18 Desemba 2025 wakati hafla ya kukabidhi magari nane kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za TOSCI na ukaguzi wa maendeleo ya ukarabati wa maabara ya Taifa ya mbegu.

Maabara hiyo inatambulika na Taasisi ya Kimataifa ya Kusimamia Miongozo ya Kufanya Majaribio ya Maabara (ISTA); huku magari 8 yaliyokabidhiwa yatatumika kuendesha shughuli za TOSCI za kukagua na kuthibitisha mbegu katika Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na mengine kuendesha shughuli za ukaguzi na kuthibitisha mbegu zinazofanywa na Makao Makuu ya TOSCI. 

“Tuna bahati sana kutumikia wakulima na ni lazima kutoa huduma za kitaalamu ili kurahisisha mavuno bora, kipato na biashara kwa wakulima,” Amesema Katibu Mkuu Mweli.

Wakati wa hotuba yake, amewakumbusha Watumishi wa TOSCI kuwa “hakuna mtu mdogo ndani ya Taasisi kwenye UTUMISHI wa Umma. Ukubwa wa mtumishi wa Umma unaendana na mwenendo wa tabia ndani na nje ya ofisi tubadilishe utaratibu wa kusubiri kupangiwa kazi. Kila mtu ana kazi za kufanya na ana nafasi ya kubadilisha au kuongeza ufanisi katika kazi husika.  Hivyo, tujitume kuwqtumikia wananchi,” amesema Katibu Mkuu Mweli. 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TOSCI, Dkt. Lilian Sechambo ametoa shukran kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwzesha utekelezaji wa ukarabati wa maabara na vitendea kazi, yaani magari ambapo Taasisi hiyo inaenda kutoa huduma kwa ufanisi zaidi kama chachu ya maendeleo kwa wakulima.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Bw. Nyasebwa Chimagu amemuhakikishia Katibu Mkuu kuwa Taasisi hiyo itaendelea kutoa elimu na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokiuka matakwa ya sheria ya mbegu na kanuni zake.

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top