Na Angela Sebastian
Bukoba; Mkuu wa mkoa wa Kagera Khajat Fatma Mwassa ameiomba Serikali kupitia wizara ofisi ya Rais maendeleo ya vijana kuwaunganisha vijana wa mkoa huo kunufaika na fursa zinazojitokeza hapa nchini na nje ya nchi ikiwemo mafunzo ,makongamano na mashindano ili kuwasaidia kufanya makubwa zaidi katika sekta ya ajira.
Mwassa ametoa ombi hilo leo kwa Naibu katibu mkuu wa Wizara hiyo Dk.Kedmon Mapana katika uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji vijana wa mkoa wa Kagera katika tamasha la Ijuka Omuka (kumbuka nyumbani) linaloendelea mjini Bukoba
Hajat Mwassa katika taarifa yake amebainisha fursa zilizotengenezwa na serikali kwa vijana wa Kagera katika kupambana na changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana ambapo ni kuhakikisha Halmashauri zote nane za mkoa huo wanazalisha ajira 2000 za vijana kila mwaka kupitia sekta ya kilimo, ufugaji, karakana na mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Serikali ya upande wake Naibu katibu mkuu wa Wizara ya ofisi ya Rais maendeleo ya vijana Dk.
Kedmon Mapana amewashauri vijana wa mkoa wa Kagera kutumia mitandao ya kijamii kutangaza mafanikio yanayotokana na mikopo ya asilimia kumi ya Halmashauri ili na wengine waweze kujitokeza na kutumia fursa hiyo kujiajiri kama walivyofanya wao.










