Na Angela Sebastian
Bukoba : Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene amewataka wanakagera waishio nje ya Kagera kurudi nyumbai ili kuwekeza ikiwa ni kuasisi tamasha la Ijuka Omuka linalowakutanisha wanakagera wote kwa maslai ya vizazi vilivyopo na vijavyo.
Amesema hayo wakati wa kufunga Tamasha la utamaduni la Ijuka Omuka ambapo amewataka wazazi wote nchini kuwafundisha mila,desturi na utamaduni wa wazee wao ili waepuke kujiingiza katika mambo yasiyofaa.
Aidha amewashauri wanakagera kufanya uzalishaji wa tija katika zao la ndizi na bidhaa nyingine zitokanazo na zao hilo pia kufanya utafiti wa ndizi zinazofaa kuzalishwa na kuzwpa nje ya nchi na kuingiza uchumi wa mkoa wa Kageta na Taifa letu
Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema lengo la Tamasha hilo ni kuirudisha Kagera kwenye uhalisia wake,kujadili maendeleo yao,kuibua fursa zilizopo na kutengeneza mikakati ya kutatua changamoto zinazoukabili wa mkoa huo.









