NHIF Yawajengea Uwezo Viongozi wa Serikali, Dini na Watoa Huduma za Afya Kagera

0


 Angela Sebastian 

Bukoba: Viongozi wa sekta mbalimbali za Serikali,dini na watoa huduma za Afya mkoani Kagera wamejengewa uelewa juu ya utekelezaji wa sheria ya mfuko wa bima ya Afya kwa wote, ikiwa ni kuanza kutekelezaji wa ahadi ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya siku 100 aliyoitoa wakati wa kampeini za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Mafunzo hayo yametolewa leo katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa kagera ambapo wamesisitizwa kutoea elimu kwa nguvu zote kwa wananchi huku wahudumu wa Afya wakitakiwa kuondokana na mazoea katika utoaji wa huduma.

Said Makola ni mratibu wa mpango wa Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote  kutoka Wizara ya Afya akizungumza katika mafunzo hayo  alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya wanao wajibu wa kutoa miongozo na tafsiri ya sheria ya bima ya afya pamoja na kanuni zake ili ziweze kutekelezwa kwa urahisi katika mikoa yote Tanzania Bara.

Alisema zaidi kaya laki  9.3 sawa na asilimia 23.7 kwa hawamu ya kwanza zimetambuliwa ambapo lengo ni kufikia kaya milioni 3.9 sawa na asilimia 26 za watu wasio na uwezo   kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ambazo zitaanza kusajiliwa muda wowote kuanzia hivi sasa.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa akiongea na washiriki hao alisema kuwa mpango huo wa bima ya Afya kwa wote ni utelekezaji wa dira ya Taifa ya mwaka 2050 kuhakilisha kila mwananchi anapata huduma stahiki

Naye meneja wa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya  (NHIF) mkoa wa Kagera  Ismail Kangeta amesema zamani wanafunzi walilipia kifurushi cha shl. 50,400 ambapo kwasasa wazazi watakapolipia 150,000 ambayo,inatakuwa inajumuisha watu sita hivyo ata watoto au wanafunzi kama ni wa familia hiyo watahusishwa.





Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top