Mhe. Hazali Awahimiza Wananchi Katesh Matumizi ya Nishati Safi na Salama ya Kupikia

0


Hanang : Mkuu wa wilaya ya Hanang Mheshimiwa Almishi Hazali ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Hanang kujitokezo kwa wingi  kununua majiko banifu ambayo yameanzwa kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku.

Wito huo umetolewa leo tarehe 20 Novemba, 2025 na Mheshimiwa Hazali alipofika katika Tarafa ya Katesh Kata ya Nangwa kijiji cha Nangwa kukagua na kufatilia utekelezaji wa mradi ambapo jumla majiko 1,583 yatasambzwa  na kuuzwa kwa bei ya ruzuku wilaya nzima.

“Mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni mwendelezo wa  juhudi za serikali  katika kutunza mazingira na kuboresha afya za  wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia”Alisema Mhe. Hazali.

Akizungumza wakati wa uuzaji wa majiko hayo, msimamizi wa mradi kutoka REA, Ndugu Abdulrazack Mkomi amesema,

Serikali imeweke ruzuku ya asilimia 80 katika  kila jiko  ili kumpunguzia mwananchi hususani wa  maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji gharama ya kununua jiko  na hivyo badala ya mwananchi kununua jiko kwa Tsh 56,000 atanunua kwa  Tsh 11,200 pekee.

Aidha, Mradi huu unakuja kubadilisha mtazamo wa wananchi katika matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kutoka kutumia kuni na mkaa mwingi  mpaka kutumia kuni na mkaa kidogo wakati wa kupika.

Majiko haya yametengenezwa kwa nyenzo ambazo zinasaidia jiko kuhifadhi joto kwa mda mrefu hivyo kupunguza matumizi makubwa ya mkaa na kuni

Aidha majiko haya hayatoi moshi na hivyo kupunguza uzalishaji wa  sumu itokanayo na kuni na mkaa ambayo husababisha magonjwa yanayochangiwa na uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba.






Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top