NEMC Yaendesha Mafunzo ya Ndani ya Tathimini ya Miradi na Athari kwa Mazingira na Jamii

0


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeandaa mafunzo ya maalum ya siku nne kwa watumishi wake wa kanda za Dar-es-salaam yenye lengo la kuwajengea uwezo juu ya mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii na Kaguzi za Mazingira ili kuwaongeza ufanisi katika mapitio ya miradi husika. 

Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi 18 Novemba 2025 na Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii (NEMC)  Bi. Lilian Lukambuzi, ambapo yanatarajiwa kuhitimishwa Novemba 21, 2025.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Bi. Lilian Lukambuzi alisisitiza umuhimu wa Sheria ya Mazingira na Kanuni za Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya 2005 na marekebisho yake(2018) na 2024 katika mchakato wa mapitio ya Miradi ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira.

Aidha, amesisitiza watumishi kujikita katika mapitio thabiti ya miradi ili kuwa na  mipango bora ya Usimamizi wa mazingira na  Ufuatiliaji itakoyeleta uendelevu wa miradi husika .

Watoa mada katika mafunzo hayo ni wataalamu waandamizi wa Mazingira wakiwemo Kaimu Meneja wa Mapitio ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii, Mhandisi Luhuvilo Mwamila na Meneja Usajili wa Wataalam elekezi wa Mazingira, Bi. Edika Masisi ambaye alijikita katika kuelezea kwa kina hatua za Tathmini ya Athari kwa Mazingira na vigezo vya kuzingitia katika mapitio ya Miradi na namna bora ya uandaaji wa ripoti za TAM na Kaguzi za Mazingira.

Chanzo: NEMC





Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top