Na Angela Sebastian
Bukoba : Mgombea Ubunge wa jimbo la Bukoba mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhandisi Johnston Mutasingwa amewashukuru wananchi wa jimbo hilo, kwa ushirikiano na mapokezi makubwa waliompatia tangu kuanza kwa kampeni za kunadi Ilani ya chama hicho na kuomba ridhaa.
Adha amewashauri wajitokeze kwa wingi kesho kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa kupiga kura na kuchagua viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya Taifa hadi kata ili waweze kushirikiana kuwaletea maendeleo.
Mutasihgwa ameeleza hayo leo wakati akihitimisha kampeni zake katika viwanja vya Shule ya Msingi Kashai ndani ya Manispaa ya Bukoba ambapo amesema kesho ni siku muhimu kwa Taifa letu hivyo, akawaomba wananchi kumuamini na kumtuma kwa kumpigia kura za kutosha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,yeye kwa nafasi ya ubunge na madiwani kwasababu ndiyo chaguo sahii la kutatua kero zao.
"Nawaomba mjitokezeni kwa wingi kesho mpige kura kwa amani, utulivu na mchague viongozi wa CCM tutumeni kwasababu uongozi siyo ajira bali ni utumishi kwa wananchi waliokuweka madarakani hivyo, sisi mkituchagua tunaenda kuwatumikia"ameeleza Mutasingwa
Kwa upande wake kampeni meneja wa mgombea huyu Amani Kajuna amewaeleza wananchi wa jimbo hilo kuwa CCM inayosabubu ya kuomba ridhaa tena kwasababu kwa kipindi cha miaka minne ya Dk.Samia ameleta zaidi ya shilingi bilioni 36 katika jimbo la Bukoba mijini kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Nao viongozi mbalimbali waliohudhulia hitimisho la kampeini hizo akiwemo mbunge aliyemaliza muda wake Stephen Byabato na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Bukoba mjini Zachwa Muganyizi wametoa wito kwa wananchi kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwao bila kujali itikadi za kisiasa.










