Angela Sebastian
Bukoba : TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Kagera imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya mapambano dhidi ya rushwa wakati wa uchaguzi na kuwakumbusha kuzingatia miiko ya kazi zao.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo Vangsada Mkalimoto ametaja lengo la mafunzo hayo kuwa ni kuwakumbusha waandishi wa habari wajibu wao wa kupambana na kuzuia rushwa pia kuelimisha jamii madhara yatokanayo na rushwa.
"Waandishi wa habari ni watu wa muhimu sana katika jamii nawashauri kuzingatia miiko ya kazi zenu za habari pia na mtumie kalamu zetu kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru,amani na haki"
Mada zilizotolewa na PCCB katika mafunzo hayo ni pamoja na wajibu wa waandishi katika mapambano dhidi ya rushwa katika uchaguzi, makosa ya rushwa katika sheria ya uchaguzi ya Rais, wabunge na madiwani namba 1/2024 na makosa ya rushwa katika sheria ya gharama ya uchaguzi namba 6/2010







