Na Angela Sebastian
Missenyi: Wananchi wa vitongoji nane wapatao 7,562 katika kijiji cha Mutukula Wilayani Missenyi mkoani Kagera wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji wa kijiji hicho, unaohudumiwa na mamlaka ya Maji safi maji taka na usafi wa Mazingira (BUWASA) ambao umefikia asilimia 70.
Mradi huo ambao unatagharimu shilingi Bilioni 1.4 utakapokamilika utaongeza upatikanaji wa maji katika eneo linalohudimiwa na BUWASA kwa wilaya hiyo kutoka asilimia 86 ya sasa hadi 100.
Kiongzi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2025 Ismail Ali Ussi umetembelea mradi huo na kulidhishwa na maendeleo ya utekelezaji ambapo amesema hayo ni maono ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi hawatembei mwendo mrefu kufuata huduma ya maji .
"Tumelidhishwa na utekelezaji wa mradi huu ambapo unahudumiwa na Buwasa tunawaomba wanachi wa vitongoji vitano ambavyo bado havijapata maji tuwe wavumilivu mradi unakamilika muda si mrefu tunapata maji safi na salama kwasababu nia ya Dk.Samia ni kumtua mama ndoo kichwani na kuondoa changamoto ya kukosa maji safi na salama"amesema Ussi.
Ameseama ujio wa mwenge wa uhuru katika mradi huo inaashiria kuwa mradi huo utakamilika.kwa wakati maana Mwenge haujawahi kusema uongo.
Mratibu wa Mradi mhandisi Lucas Selebeya meneja Buwasa wa Wila ya Missenyi, wakati akitoa taarifa kwa Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa juu ya maendeleo ya mradi amesema mradi ujenzi ulianza Januari 2025 umefikia asilimia 70 ambapo vitongoji vitatu kati ya nane vinapata huduma ya maji safi na salama unatarajiwa kukamilila Desemba 30 mwaka huu na kugharimu shl bil.1.4
Thadeo Kashalala ni mmoja wa wananchi ambao tiyali wameishaunganishiwa huduma ya maji anasema wanashukuru Serikali kwa kuleta mradi huo, kwani walikuwa wakitumia maji machafu kutoka kwenye madimbwi ambayo wananyweshwa mifugo huku wakati wa kiangazi walitembea kilometa 10 kufuata maji mto Kagera.