Na Angela Sebastian
Missenyi: Mwenge wa uhuru umezindua bweni la wasichana wa kidato cha tano na sita lenye vyumba viwili katika shule ya sekondari Kyaka iliyoko Wilayani Missenyi mkoani Kagera.
Bweni hilo ambalo limegharimu shillingi milioni 260 ambapo ni chachu kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike wanaotarajiwa kujiunga na shule hiyo mwaka kesho, kufanya vizuri katika masomo yao,kujiamini na kuepuka adha za kiusalama ambazo watoto wa kike hukumbana nazo wanapotafuta elimu.
Akisoma taarifa ya mradi kwa kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ismail Ali Ussi leo,mkuu wa shule hiyo Fadhir Nnko amesema fedha ya ujenzi huo ilitoka Serikali kuu ambapo mradi huo ulianza kutekelezwa Machi 15,2025 na kukamilika Agosti 20 mwaka huu kwa asilimia 100.
"Bweni hilo linaouwezo wa kulaza wanafunzi 160 wa kidato cha tano na sita kwa wakati mmoja ambao wanatarajiwa kudahiliwa mwaka ujao wa masomo kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na itasaidia kuondoa adha za watoto wa kike kutembea umbali mrefu kuja shule na kuepukana na changamoto za kuwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia"amesema Nnko.
Naye kiongozi wa mbio za mwenge Ismail Ali Ussi amesema popote palipojengwa miundombinu bora ya sekta ya elimu lazima watoto wanasomaw
"Rais Dk Samia Suluhu Hassan aliona ipo haja leo hii kuwa wapo wanafunzi ambao wanapokaribia kipindi cha mitaihani hutembea kipindi cha masafa marefu kuja kupata huduma hiyo ni kutengeneza uduni wa wanafunzi hao"amesema Ussi
Amesema uduni huo unatokana na kwamba mwanafunzi anapotembea umbali wa mita 500 kilometa moja au masaa mawili hadi matatu alafu, arudi nyumbani kwa masaa hayohayo na wakati mwingine anakabiliwa na kipindi cha mitihani kwakweli hapo unakuwa hujatengeneza elimu bora ya mwanafunzi huyo.
"Hapo hujui njiani atakumbana na nini,atakutana na vishawishi gani ambavyo vinamtoa katika suala zima la kupata elimu kwahiyo ndiyo maana Dk.Samia akaona ipo haja sasa ya kujenga mabweni maalum kama haya ambao ni moja ya shule hizo ili watoto waweze kubaki shuleni na kuepukana na adha hizo"ameeleza Ussi
Naye mkuu wa Wilaya ya Missenyi kanali mstaafu Hamis Maige wakati akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima amesema mwenge utakagua,utatembelea na kuweka mawe ya msingi Katika miradi saba yenye thamanj ya shilingi bilioni 2.4