Hamasisheni Wananchi Juu ya Matumizi ya Nishati Safi - Ismail Ali Ussi

0


 Na Angela Sebastian 

Biharamulo: Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ismail Ali Ussi amewataka mkuu wa mkoa wa Kagera,wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote na Manispaa ya Bukoba   kuwahamasisha wananchi kutumia Nishati safi ili kuepukana na athari za kiafya zitokanazo na nishati chafu.

Ametoa ushauri huo akiwa Wilayani Biharamulo ambapo amesema viongozi hao wanakumbuka kwamba Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekuja na kampeni ambayo ina lengo la kuwasaidia wananchi wa Tanzania ikiwemo Biharamulo ambapo inaenda kuwajali na kuwagusa wananchi moja kwa moja kwa kuweka Afya zao kuwa imara.

"Dk.Samia amekuja na utaratibu wa uhamasishaji wa matumizi ya gesi na Nishati safi mbadala katika maeneo mbalimbali ndani ya Taifa hili ,ndiyo maana yapo maelezo yaliyotolewa kwa wakuu wa mikoa,Wilaya na wakurugenzi kuwataka wahamasishe kampeni hiyo katika maeneo ambayo yana mkusanyiko wa kuanzia watu 100 na kuendelea  ikiwa ni ya binafsi au Serikali kuhakikisha wanatumia gesi ambapo shule yss Biharamulo (A) imeonyesha kuunga mkoni zoezi hilo kwa vitendo .

Amesema Serikali katika kampeni ya nishati safi ilifanya utafiti wa kina,baada ya kugundua kwamba wananchi waliowengi leo hii wanaathirika Afya zao kutokana na matumizi ya nishati chafu ya kuni ya kupikia jambo ambalo, huwezi kujua usalama wa Afya yako kwa wakati huo mpaka baada ya miaka miwili kwani inaenda kuhimidi muda mrefu na ikizidi kudhoofisha Afya ndani ya miili yetu hapo ndipo tunaanza kupata shida ikiwemo kukohoa ovyo.

"Ndiyo maana Serikali imewekeza huko matarajio ya kampeni hiyo ya Dk.Samia yakiwa ifikapo mwaka 2030 zaidi ya asilimia 80 ya watanzania waweze kutumia Nishati safi 

Benson Mwamelo ni afisa misitu  Wilaya ya Biharamulo akitoa taarifa   kwa kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ismail Ali Ussi juu ya mradi wa Nishati safi katika shule ya msingi Biharamulo (A) yenye kitengo cha elimu maalum   amesema Wilaya hiyo wanaendelea kuwasaidia wananchi na kuhakikisha   wanatumia nishati safi ambapo ni njia moja wapo ya kukabiliana na matumizi ya mkaa na kuni.

Amesema Halmashauri hiyo imetoa zaidi ya  shilingi milioni 9 kutokana na mapato ya ndani ambapo zimetumika kwa ajili

ya kufunga  majiko mawili ya kisasa sufuria zinazotumika kwenye kupikia mitungi minne ya gesi na kufunga miundombinu yake ambayo ni kuunga mkono kampeni ya Serikali ya matumizi ya Nishati safi kwa vitendo.

Naye mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Advera Bulimba amesema Mwenge wa Uhuru umezindua,kukagua na kuweka mawe ya msingi Katika Miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni mbili  ikiwemo elimu Afya,barabara,maji na Nishati safi. 







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top