Mradi wa Kilimo cha Parachichi Kuchochea Ukuaji wa Uchumi kwa Vijana - NGARA

0




Na Angela Sebastian 

Ngara: Kikundi cha vijana wapatao nane wa Kata ya Kabanga Wilayani Ngara mkoani Kagera ambao wamejiunga pamoja na kuanzisha kilimo cha matunda aina ya Parachichi wamekuwa kichocheo cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi ambapo huwaingizia kipato.

Utekelezaji wa Sera ya vijana ya mwaka 2017 hadi 2034  imeisukuma Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kutenga shilingi milioni 52.6 na kati ya hizo ml.40 ikiwa ni asilimia 10 itokanayo na mapato ya ndani huku vijana wenyewe kutokana na Sera hiyo wakichangishana fedha taslimu kupitia kikundi chao na kupata shl.mil 200.

Mwenyekiti  wa kikundi hicho cha Kabanga matunda group,Livingstone Shedrack ametoa taarifa kwa Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ali Ussi na kusema kuwa lengo la vijana hao kwa kushirikiana na Halmashauri ya Ngara ni kuhakikisha vijana wanajipatia ajira na kipato pia mradi huo hutumika kujinfunza kilimo cha parachichi kutafuta masoko ili kuuza na kupata faida.

 Shedrack amesema mradi huo wenye ekari 24.05 umegharimu zaidi  ya shilingi milioni 252.6 ambapo shl. mil.200 zinatokana na maamuzi ya wanakikundi wanane kuamua kuanzisha mfuko wa kuweka na kukopa ili waanzishe mradi utakao wainua na kuondokana na umaskini huku mil 52.6 ikitoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara .

"Manufaa ya mradi huu vijana 200 kutoka ndani ya kata ya Kabanga wamepata ajira ambapo inawasaidia kujiongezea kipato,kusaidia watu wenye mahitaji maalum ikiwemo watoto na wazee,tumekuza biashara zetu kwa kuanzisha vituo vitano vya ukusanyaji wa parachichi kutoka sehemu mbalimbali na kuwauzia wafanyabiasha wakubwa"ameeleza Shedrack .

Msafiri Joseph na Nickson Nicodemas  ni wanakikundi wanasema matamanio yao ni kuona kila kijana aliyeko nje ya kikundi anajiunga na  anapata fursa hiyo ya kujiajiri kwasababu wao walianza wakifanya kazi za vibarua kwa matajiri kwa kukusanya parachichi hari iliyowafungua akili kuwa na wao wanaweza kujiajiri.

 Pia wamemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kiuchumi na kufikia malengo yao .

Naye kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ussi wakati akizindua mradi huo amepongeza ubunifu wa vijana hao na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono ili wafikie malengo yao kwasasa hayo ni matamanio makubwa ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuona vijana wanajiingizia kipato kwa njia halali.

Mkuu wa Wilaya ya Ngara kanali Mathias Kahabi amesema Mwenge umezindua  miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 2.7.















Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top