Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Uwekezaji (TISEZA) imesaini makubaliano na Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) kwa ajili ya kutoa huduma za kifedha kwa wawekezaji leo Septemba 20, 2025 katika ofisi za Makao Makuu ya TISEZA.
Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA Bw. Gilead Teri TCB amesema kuwa TCB ni benki inayokua kwa kasi, tunaamini itarahisisha huduma kwa wawekezaji wetu pamoja na kushirikiana katika kuhamasisha Uwekezaji Nchini.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB Bw. Adam Mihayo amesema kuw benki hoyo iko tayari kusaidia wawekezaji na kupanua huduma zaidi na kushirikiana kwa kwa karibu na TISEZA kwa lengo la kuongeza ufanisi.
Makubaliano haya ni sehemu ya juhudi za kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kushirikiana taasisi za umma kwa maendeleo ya Taifa
Chanzo: TIC