NEMC Yashiriki Wasilisho la Ripoti ya Makundi Maalum Kutoka kwa Asasi ya Wanted Jijini Dodoma

0


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeshiriki uwasilishaji wa ripoti ya mchango wa wanawake, wasichana na makundi yaliyo pembezoni kwenye sera ya Taifa ya Ardhi 1995 (Toleo la 2023) na mchakato wa NDC 3.0V  uliofanyika katika ukumbi wa Residence Jijini Dodoma leo.

Akiwasilisha ripoti hiyo iliyoandaliwa kwa kushirikiana na WAHEAL na  Tree of Hope, Mkurugenzi wa Asas ya Kiraia kutoka Women Action Towards Entrepreneurship Development (WATED) Bi.Maria Matui amesema imelenga kuainisha changamoto za wanawake wa vijijini pamoja na kusaidia jitihada za mashirika katika kupaza sauti za wanawake kwenye masuala ya usimamizi wa ardhi na harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.  

Amesema wasilisho hilo lililohusisha pia wanachama wa mtandao wa mabadiliko ya tabianchi limeainisha changamoto nyingi wanazopitia wanawake wa vijijini zikiwemo, mila na desturi, mitazamo na mifumo dume hali inayoathiri masuala ya maendeleo hasa shughuli za uzalishaji.

Malengo makubwa matatu yaliyowasilishwa ni pamoja na kuweka wazi mchango wa wanawake, wasichana na makundi yaliyo pembezoni katika utekelezaji wa Sera ya Ardhi ya 1995(Toleo la 2023, kushirikiana na Serikali katika kuboresha mchakato wa NDC.3.0V kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na haki za makundi yote ya jamii pamoja na kutoa mapendekezo Sera shirikishi yatakayohakikisha usimamizi endelevi wa rasilimali na upatikanaji wa haki sawa kwa kila mmoja.

Mikoa iliyofikiwa na Asas hizi ni pamoja na Ruvuma, Morogoro, Kilimanjaro, Geita, Arusha, Mara, Kagera na Tanga.

Chanzo: nemc





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top