Kiwanda cha Kusafirisha Graphite Godmwanga Tafsiri ya Tanzania ya Viwanda

0


 

📌Kampuni Inauwezo wa Kuchakata Zaidi Tani 1000 kwa Siku kwa Ubora wa 95%

📌Soko Lake Lipo Marekani, China na Korea Kusini*

📌Ni Kiwanda cha Kwanza cha Graphite Nchini*

Handeni: Wakati dunia ikipiga hatua kuelekea kupunguza matumizi ya nishati inayozalisha hewa ukaa na kuongeza matumizi ya nishati safi, viwanda vya kusafisha madini ya kinywe (graphite) vya Godmwanga Gems vinaibuka kuwa tafsiri ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda na jinsi madini yanavyochochea ukuaji wa viwanda Tanzania.

Viwanda hivyo viwili vinavyopatikana katika Vijiji vya Kwedikabu na Kwamsisi Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga,  vinamilikiwa na Mtanzania Godlisten Mwanga, kwa asilimia 100 na kutumia rasilimali za madini za Tanzania, kwa kuchakata na kugeuza kinywe ghafi kuwa tayari kwa matumizi ya viwandani.

Viwanda hivyo ni vya kwanza nchini Tanzania kuanza uzalishaji wa madini Kinywe na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu barani Afrika baada ya Madagascar na Msumbiji na kuhakikishia nafasi ya Tanzania kama kiungo muhimu katika usambazaji wa bidhaa hiyo muhimu duniani. 

Septemba 08, 2025, Akizungumza na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Madini, Meneja wa Kiwanda B, Henry Joseph alieleza kuwa, kuanzishwa kwa viwanda hivyo kumesaidia kuimarisha nafasi ya Tanzania katika uchumi wa kijani (green economy) kutengeneza ajira kwa wenyeji, utengenezaji na ukarabati wa miundombinu ya afya, elimu, barabara, ukuaji wa kiuchumi sambamba na kuonesha jinsi madini yanavyoweza kuwa nguzo muhimu ya ukuaji wa viwanda nchini.

Uwekezaji wa Viwandani na Teknolojia*

Viwanda vya Godmwanga vina uwezo wa kuchakata na kusafisha graphite hadi kiwango cha juu cha asilimia 95 kinachokubalika kimataifa. Hatua inayofanya Tanzania kuwa msambazaji wa malighafi muhimu kwa sekta kama betri za umeme, vifaa vya kiteknolojia na vilainishi vya viwandani, mashine muhimu na magari hivyo kuwa sababu ya kuanzishwa kwa viwanda vingine vinavyotegemea malighafi hizi.

Ajira, Mafunzo, na Uwezo wa Jamii

Kupitia mafunzo ya kazi, mafunzo ya ufundi, na mpangilio wa usalama kazini, wakazi wa Kata ya Kwamsisi.

Chanzo: wizara ya madini



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top