Mkoa wa Kagera Wapokea Miradi ya Kinga Dhidi ya VVU na Uwekezaji kwa Wasichana na Wanawake

0


 Na Angela Sebastian

Bukoba : SERIKALI ya mkoa wa Kagera imepokea miradi miwili ya kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi (VVU) kupitia tohara kwa wanaume na wavulana (VMMC) na uwekezaji kwa wasichana na wanawake (Dreams) ambayo ilikuwa inafadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Afya ya jamii katika kuzuia VVU,huduma na matibabu (MDH).

Akipokea miradi hiyo  kwa niaba Serikali,katibu tawala msaidizi utawala na rasilimali watu Bwahi Biseko mjini Bukoba amesema, miradi hiyo aliyoipokea ilikuwa ikidhaminiwa kupitia mpango wa dharula wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR) ambayo kwanza ni mradi wa tohara ambao umefikia  wanaume na wavulana 539,835 katika mkoa wa Kagera.

Amesema takwimu hiyo ni  sawa na asilimi 95 ya waliolengwa tangu mwaka 2016 hadi sasa toka mradi huo ulipoanzishwa kwa lengo la kupambana na maambukizi mapya ya VVU ambapo Serikali imejipanga vyema kuiendeleza.

"Sasa kama tumekwishaingizwa katika huduma za kawaida inamaana tunatakiwa kuzingatia mifumo iliyopo katika kuhakikisha kwamba tunandelea na huduma za tohara ili kuhakikisha huduma zinapatikana na kutolewa kama ilivyokuwa kabla ya mfadhiri kumkabidhi miradi hii kwetu"

 Amesema amefuatilia na kuambiwa kuwa sasa huduma iko chini sana  ukiangalia vituo vilivyokuwa vinajaza watu wakati wa mradi huu kutokana na huduma kuwa bure ambapo takwimu ya mwezi walikuwa wakitoa huduma kwa watu 200 hadi 500 sasa hivi wana takwimu ya moja au mbili.

Amesema hicho ni kiashiria kwao kama viongozi na watekelezaji wa huduma kwenda kuzingatia kwa kupambana na yanayowarudisha nyuma kwa kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu na inaendelea kutolewa kwa watu wa mkoa wa Kagera.

Amesema Serikali imeishajipanga kuendeleza miradi hiyo kutoa huduma stahiki kama ilivyokuwa hapo awali bila kukwama hivyo akawashauri wananchi kuondoa wasiwasi na hofu ya kukosa huduma.

Adha amesema kuwa mradi wa wasichana na wanawake kujikwamua kiuchumi na kupunguza athari ya mambukizi ya VVU kwa kuboresha maisha yao wa dreams umefikia wanawake na wasichana wapatao 54,000 wa Manispaa ya Bukoba na Muleba.

Amesema mradi huo umesababisha kupiga hatua kubwa ambapo tangu miaka sita ulipoanzishwa mpaka sasa wameanzisha  miradi mikubwa inayowafanya watumie muda mwingi kijishughulisha kuliko kujiingiza katika vishawishi vinavyoweza kuwaingiza katika maambukizi ya VVU.

Pia amewataka vijana walioko katika mradi wa huo kutengeneza na kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kwendana na ushindani wa soko la sasa.

Kwa upande wa MDH kutoka makao makuu Dk.Emmanuel Sima amesema katika mradi huo asilimi 60 ya waliotahiriwa walitafutwa kupitia maeneo mbalimbali na asilimi 40 wakifika kwenye vituo vya kutolea huduma.

Aidha amesema kukabidhiwa kwa miradi hiyo miwili kwa Serikali siyo mwisho wa utoaji huduma za MDH katika mkoa wa Kagera, bali wataendelea kuwepo na  kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutoa huduma mbalimbali katika sekta ya afya kama ilivyo kawaida yao.

Leonida Rweyemamu ni mmoja wa wauguzi walioanza na mradi wa Tohara mwaka 2016 ulipoanzishwa ameeleza kuwa wakati mradi unaanza jamii haukupokea huduma hiyo 

kwa usahii kutokana na imani na mira zao kwamba mwenye wajibu wa kutahiriwa  ni lazima awe muislam.

"Tulipowafuata baadhi ya wanaume waliowengi walisema nchi imekuja na mbinu ya kubadilisha watu kuwa waislam hivyo hari hiyo ilisababisha kukosa wateja, naipongeza juhudi za MDH na Serikali walibuni njia mbalimbali za kutoa ujumbe kupitia vyombo vya habari,mikutano ya adhara,kuongea na vijana shule,viongozi wa dini na Serikali kuelimisha jamii"amesema Rweyemamu 

Amesema wanaume walifundishwa kuhusu faida za kutahiriwa ikiwemo kupunguza maambukizi ya VVU kwa asilimia 60,usafi na kusaidia akina mama kuepuka kupata kansa ya kizazi hivyo, siku zilivyokuwa zinaenda ndivyo wateja waliongezeka ambapo kwa mwezi waweza kutahiri wanaume na wavulana kati ya 200 na kuendelea waliofika vituoni na waliiofuatwa katika maeneo kupata huduma.

Adelitus Mulokozi ni mkazi wa Manispaa ya Bukoba mmoja wa wanaume waliopata tohara kwa kipndi cha mradi huo amesema wao tangu wakiwa watoto walielezwa kuwa mwanaume anayetahiriwa ni wa dini ya kislam hari iliyosababisha wanaume wa mkoa huo walio wengi kutopata huduma hiyo kama ilivyo kwa mikoa mingine.

"Nashukuru Serikali na wadau wetu wa MDH kuleta huduma hii ambapo  tulielimishwa mimi, nilipata kujua faida za tohara hivyo nikashawishika na kujitokeza pia vijana wangu wawili nao niliwapeleka kisha kupata huduma hiyo kwanza inasaidia kupunguza maambukizi ya VVU kwa kiwango kikubwa pia inasaidia wake zetu kuepukana na maambukizi ya saratani ya kizazi "ameeleza Mulokozi 

Dilica Deogratias ni binti ambaye amenufaika na mradi wa dream baada ya kupata elimu kupitia kituo kilochotengwa cha Sido Kagera ambapo kwa sasa anaweza kutengeneza sabuni na batiki na kuuza kisha kujiingizia kipato.

"Mradi wa dream umenisaidia kuepuka na utegemezi na ombaomba kwa ndugu,jamaa na marafiki ambapo wengine hawana nia nzuri pia kuepukana na vishawishi vinavyoweza kuniingiza katika mazingira yasiyo mazuri ambayo yanasabisha kujiingiza katika ngono zisizo salama"ameeleza Deogratias

Amesema kwasasa anatumia muda mwingi na wanakikundi wenzake kuzalisha na kutafuta wateja kwa ajili ya bidhaa zao hari inayowasaidia kujiepusha na maambukizi ya VVU.











Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top