Na Angela Sebastian
Kyerwa: Katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kupambana na uhalibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi mwenge wa uhuru umezindua kitalu cha miche zaidi ya milioni 1.5 kinachomilkiwa na mwekezaji wa mzawa Lenard Kachebonao katika kijiji cha Kitwe Wilaya Kyerwa mkoani Kagera.
Kitalu hicho chenye aina 13 za miche tofautitofauti ikiwemo kahawa,mbao viungo na matunda kiko katika kijiji cha Kitwe Wilayani humo ambapo miche hiyo hugawiwa kwa wananchi wa mkoa wa Kagera na mikoa jirani ili kupandwa na kuzalisha hewa ukaa ambayo ni njia ya kutunza mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Kachebonao amemueleza kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Ussi alipokuwa alitembelea mradi huo kuwa nia yake ni kuunga mkono jitihada na maono ya Dk.Samia ya kuhakikisha Tanzania inakuwa kinara dunia katika utunzaji wa mazingira hivyo na yeye aliamua kunzisha mradi huo ambao mbali na kutunza mazingira wananchi wanapata matunda na kuboresha Afya zao.
Naye kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Ismail Ali Ussi amesema Dk.Samia anaunga mkono juhudi za wawekezaji kama hao ambapo huzalisha miche ya matunda na ile ambayo hutumika katika matumizi ya kila siku kwani huwasaidia wakulima kupata miche bora na kisasa maana mwekezaji huo ameonyesha upendo mkubwa kwa jamii.
Wakati huo huo Ussi amegawa Mitungi 514 ya gesi kwa akina mama wajasiriamali,wenye ulemavu na taasisi,lengo likiwa ni kutelekeza kampeni na mpango endelevu wa Rais Dk.Samia ya kuhimiza matumizi ya Nishati safi ili kuondoa ukataji wa misitu na uhalibifu wa mazingira pia kuboresha Afya kwa kuondoa moshi wa kuni.