Na Angela Sebastian
Kyerwa: Wananchi wa kata Mabira Wilayani Kyerwa wameipongeza serikali kwa kuanza ujenzi wa Barabara ya Nkwenda - Mabira kwa kiwango Cha Lami ambapo wamesema kuwa mradi huo ukikamilika wataongeza wateja wa kununua mazao yao na kurahisisha usafirishaji wa mazao.
Ramadhan Robert na Bosco Gabriel wakazi wa Mabila wamesema wamekuwa wakikutana na Athari za vumbi na mali zao kuchafuka hali inayosababisha kukosa soko hasa mazao yakijaa vumbi,ujio wa mradi huo kama wafanyabiashara umewapa matumaini ya kuuza bidhaa zao zikiwa safi.
Meneja wa TARURA wilaya ya Kyerwa Yezron mbasha amesema kuwa mradi huo umegharimu kiasi Cha shilingi Milioni 471.3 ikiwa ni fedha ya Serikali inayotokana na Tozo za Mafuta.
Amesema kukamilika kwa Mradi huo kutaongeza Adhi ya mji wa mabira na Kusaidia usafirishaji wa mazao kutoka katika eneo hilo hadi maeneo mengine ya wilaya hiyo na wilaya jirani.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ussi amewataka wananchi kutunza na kulinda Miradi hiyo huku akiipongeza TARURA kwa kutekeleza miradi yenye Viwango na yenye ubora ikiwa ni pamoja kuongeza kasi ya upatikanaji wa Barabara za lami katika vijiji na maeneo yanayokua kwa Kasi.