Ismail Ali Ussi Awashauri Wananchi Kyerwa Kuacha Tabia ya Kutunza Fedha Majumbani

0



 Na Angela Sebastian 

Kyerwa: Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Ismail Ali Ussi amewashauri wananchi wa kata ya Nyakatuntu Wilayani Kyerwa mkoani Kagera kuacha tabia ya kutunza fedha majumbani ili kuondokana na mivutano inayoweza kuhatarisha usalama na amani katika jamii.

Mwenge wa uhuru mwaka 2025 umezindua tawi la benki ya CRDB la Nyakatuntu ambalo limegharimu shilingi milioni 358 ambapo litahudumia wananchi wa zaidi ya kata 10 za Wilaya hiyo.

Akiongea na wananchi waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kusikiliza ujumbe wa mwenge,Ussi amesema kuanzishwa kwa tawi hilo ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya hawamu ya sita kwani Crdb wameisha wekeza katika miradi kama hiyo maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo lengo ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu 

Amesema zile asilimia 10 zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya uhaulishaji kwa wananchi zinapitia kwa wenzetu wa Crdb kwani wao ndiyo wameweza kufunga mikataba na Serikali hivyo hakuna mwananchi atakayekosa huduma akifika katika kituo hicho.

"Wananchi wengi wa Nyakatuntu ni wakulima,wafanyabiasha na wafugaji hivyo mnauza bidhaa na kupata fedha, nawashauri tuondokane na kutunza fedha majumbani na vikundi vya mitaani njooni benki mkafungue akaunti na kuweka fedha zenu sehemu salama"

Amesema wanapaswa kufanya hivyo kwasababu ya kuendelea kulinda amani iliyopo maana kuweka fedha ndani ya nyumba pindi ikipotea watu wanaaanza kugombana na kusababisha migogoro na mifarakano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo inaweza kuhatalisha amani.

Amesema kwa niaba ya wakimbiza mwenge Kitaifa katika miradi ambayo imetembelewa na mwenge mbapo Kagera ni mkoa wa 26 mradi wa ujenzi wa tawi hilo la Crdb ni baba lao kwani wameonyesha kwa vitendo falsafa ya mwenge wa uhuru.

Kwa upande wa mkurugenzi Mtendaji wa banki ya Crdb Plc Boneventure Paul amesema kuanzishwa kwa mradi huo ni kurahisisha hupatikanaji wa huduma za kifedha,kupunguza umbali uliokuwepo,kutoa ajira,kuongeza kipato kwa jamii,mapato ya Serikali kupata kodi,ushuru wa huduma na kuongeza usalama wa utunzaji fedha kwa wananchi na Serikali. 

Jovini Jacob na Selestina Samsoni ni wanachi wa eneo la Mugakolongo wanasema walikuwa wakitembea umbali wa kilometa 17 kwenda kata ya Nkwenda kufuata huduma za kifedha na wakipanda pikipiki nauli ni kati ya shl 5000 hadi 6000.

Jacob amesema kujengwa kwa tawi hilo kutawasaidia kutunza fedha zao kwa usalama tofauti na walivyokuwa wakifanya siku za nyuma ambapo walitunza fedha ndani na kisha kuibiwa au kutapeliwa na kusababisha uvunjifu wa amani kati ya ndugu ikiwemo kipigana na kuumizana.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top