Chatanda Awaomba Wananchi Kuwachagua Wagombea wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara

0


Na Ghati Msamba

Mara: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda, ameongoza timu yake kufanya ziara mkoani Mara kwa ajili ya kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani katika wataongoza kipindi Cha mwaka 2025-2030.

Akizungumza akiwa katika Jimbo la Bunda Mjini, Chatanda alisema lengo la ziara hiyo ni kuwaombea kura wagombea wa chama hicho na kushirikiana na wanawake kuhakikisha wanashinda kwa kishindo, hususani wanawake wanne waliopitishwa kuwania ubunge katika majimbo manne mkoani Mara.

Aliwataja wagombea hao kuwa ni Esther Bulaya (Bunda Mjini) Mwita Getere (Jimbo la Bunda vijijini), Kange Lugola (Mwibara), Mgore Miraji (Musoma Mjini) na Esther Matiku (Tarime Mjini).

Chatanda aliwaasa wanawake kuhakikisha wanakiunga mkono CCM na si mtu mmoja mmoja, kwa kuwa ushindi wa chama hicho ndio utakaowasaidia kufanikisha maendeleo yao.

Alibainisha kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alihakikisha amani na utulivu vilidumu wakati wa msiba wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli, na alipoapishwa aliwaahidi kuwamilishia miradi yote ya mikakati kama miradi SGR, ulivyokuwa imefikia asilimia 20, bwawa la maji la  mwl.nyerere, baadhi ya mitandao ya Barabara za lami na ujenzi wa madarasa.






























Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top