Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA), Bw. Gilead Teri, ametoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya kuwekeza kwenye Eneo Maalum la Kiuchumi la Buzwagi, mkoani Shinyanga.
Akiwa kwenye ziara katika eneo hilo, Teri amesema eneo hilo limetengwa mahususi kwa ajili ya wawekezaji wa viwanda, hasa vinavyohusiana na madini na vifaa vya viwandani. Aidha ametumia ziara hiyo kuzungumza na wawekezaji waliowekeza katika eneo hilo.
‘Tumekuja kukagua na kuhamasisha. Eneo hili liko wazi kwa uwekezaji wa viwanda vya madini na uwepo wake unaweza kuvutia viwanda vingine pembezoni,” amesema Teri.
Fursa hii ni muhimu kuongeza ajira, kukuza uchumi wa Shinyanga na taifa kwa ujumla.
Watanzania wenye ndoto ya kuwa na viwanda – ndio wakati wenu huu!
Chanzo: TIC