Serikali ya Tanzania Yajivunia Kutekeleza Miradi ya Elimu ya Watu Wazima kwa Mafanikio

0


Serikali ya Tanzania inajivunia kutekeleza miradi mbalimbali kwa mafanikio ikiwemo, mradi wa elimu ya Sekondari Nje ya Mfumo Rasmi, ambapo katika mwaka wa masomo 2025 wanafunzi wapatao 18,886 wavulana 8,648 Wasichana 10, 239 wamedahiliwa.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kimataifa na Juma la Elimu ya Watu Wazima Septemba 19, 2025, akimwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Mhe. Mrindoka ameongeza kuwa mkakati wa kuwarejesha shuleni Wanafunzi waliopata mdondoko kwa sababu mbalimbali, ambapo zaidi ya Wasichana 13,000 wamenufaika na mpango huo.

Aidha, amebainisha kuwa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio Nje ya Shule (IPOSA) umewanufaisha vijana 12,000, wakiwemo wavulana 5,406 na wasichana 6,594 kwa mafunzo ya muda mrefu. Wanufaika wa mafunzo ya muda mfupi ni 30,183.

"Nimefurahi kusikia miongozo ya program ya Mpango wa Uwiano ya Elimu ha Watu Wazima na Jamii (MUKEJA) imezinduliwa, kwani  itasaidia kupunguza idadi ya Watu Wazima wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu" Alisema Mhe. Mrindoka.

Ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kutekeleza Kwa ufanisi miradi na program za Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.

Chanzo: wizara ya elimu






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top