Mgore Miraji Kigera ameongoza kura za Maoni Kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Katika Jimbo la Musoma Mjini Kwa kupata kura 2,255 huku Juma Mokiri akishika Nafasi ya pili Kwa kupata Kura 1,543.
Akitangaza Matokeo hayo Leo 4 Agosti 2025, katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Musoma Mjini Burhan Ruta, Amewataja wagombea wengine kuwa ni Eliud Tongora Esseko(Mkorea) Kura 115, Mashaka Nelson Biswalo Kura 44, John Kyabwe Bwana Kura 43 pamoja na Philbert Korogo Sasita Kura 34.
Amesema wajumbe Kutoka katika kata 16 za Jimbo la Musoma Mjini waliojitokeza Kupiga Kura ni 3796, Kura zilizoharibika ni 62 na Kura halali ni 3734.