Waziri Kikwete Azindua Maonesho ya Ajira Kati ya Tanzania na China

0


 Na Ghati Msamba,Dar es salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameongoza uzinduzi wa Maonyesho ya Nne (4) ya Ajira kati ya Tanzania na China, yaliyofanyika katika Viwanja vya Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, jijini Dar es Salaam.

Maonyesho haya yamelenga kuwaunganisha vijana wa Kitanzania waliomaliza masomo na wale wenye ujuzi na makampuni ya Kichina yanayofanya kazi hapa nchini, ili kuwapa fursa za ajira na kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na China.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Kikwete alisisitiza umuhimu wa kuenzi na kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili, akibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk.

 Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto ya ajira nchini.

“Maonyesho haya ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kupambana na tatizo la ajira. Kupitia maonyesho haya, makampuni ya China yanayofanya kazi hapa nchini yanawasilisha mahitaji yao ya kitaaluma na ujuzi, ili vijana wa Kitanzania wenye sifa waweze kuchangamkia fursa zilizopo,” alisema Mhe. Kikwete.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, maonyesho hayo yanatarajiwa kutoa zaidi ya ajira 2,000 kwa vijana wa Kitanzania, hatua inayochochea maendeleo endelevu na kuwajengea vijana uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.

Aidha, alitoa hakikisho kwa Watanzania kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu itaendelea kuratibu kwa ufanisi masuala ya ajira nchini, huku ikizingatia maslahi mapana ya Watanzania kwa kuongozwa na sheria, sera, miongozo ya ajira na kazi pamoja na maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top