Serikali Yatoa Msaada wa Vifaa Kwa Wanafunzi Wenye Ulemavu Singida

0


 Na Ghati Msamba-Singida.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema kuwa kauli ya "Kutoa ni moyo, si utajiri" si maneno tu, bali ni vitendo vinavyoendelea kuonekana wazi katika uongozi wa Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Kikwete aliyasema hayo  wakati akikabidhi viti mwendo na fimbo nyeupe 100 kwa wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika Chuo cha Sabasaba, kilichopo mkoani Singida. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Kikwete alisema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) tangu kuanzishwa kwake. Alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha muongo mmoja.

“Katika kipindi cha miaka kumi, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi umepiga hatua kubwa katika kuwahudumia wafanyakazi waliopata changamoto kazini. Aidha, katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Awamu ya Sita, serikali imefanya maboresho ya sera na sheria ambapo kwa sasa fao jipya la utengemao linawanufaisha watumishi wa umma wanaokumbana na changamoto za kiafya kazini,” alisema Mhe. Kikwete.

Aidha, alieleza kuwa serikali imefanikiwa kuongeza viwango vya chini na vya juu vya malipo ya pensheni, ambapo sasa fidia inaweza kufikia hadi shilingi milioni 8.4, kulingana na aina ya tukio au ulemavu.

Waziri Kikwete aliongeza kuwa mafanikio hayo yamewezesha WCF kupata ithibati ya kimataifa ya ubora wa huduma (ISO certification), jambo linaloashiria kuwa taasisi hiyo imepitia mageuzi makubwa katika utendaji yake was kazi.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top