Je, wajua taarifa zinazotumwa bila ridhaa ni nini?
Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, kifungu cha 20 kinaeleza kuhusu ujumbe unaotumwa bila ridhaa ni taarifa au data za kielektroniki ambazo hazijaombwa na mpokeaji pamoja na adhabu yake endapo mtu atakua ametenda kosa na kutiwa hatiani;
20.-(1) Mtu ambaye kwa nia ya kutenda kosa chini ya Sheria hii:-
(a) hataanzisha usambazaji wa ujumbe unaotumwa bila ridhaa;
(b) hatarusha tena au kusambaza upya ujumbe unaotumwa bila ridhaa;
(c) hataghushi ujumbe wa utambulisho na kutuma bila ridhaa.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “taarifa zinazotumwa bila ridhaa” maana yake ni taarifa au data za kielektroniki amabazo hazijaombwa na mpokeaji.
#MusomaCheck
#Chunguza kabla ya kutuma. Fikiri kabla ya kusambaza


