Wenfurebe Foundation Warejesha Matumaini kwa Familia Zilizokata Tamaa Muleba

0


Na Angela Sebastian 

Kagera : Familia mbili wilayani Muleba, mkoani Kagera, ambazo zilikuwa zikikabiliwa na changamoto kubwa za kiafya na hali ngumu ya maisha, zimepata mwanga mpya baada ya Taasisi ya Wenfurebe Foundation kutoa msaada wa jumla ya shilingi milioni nne kwa ajili ya matibabu. 

Msaada huo umetolewa kupitia Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Simon Patrick Wenfurebe, kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa hao kupata matibabu yaliyokuwa nje ya uwezo wao.

Miongoni mwa walionufaika ni Stewart Onesmo, mkazi wa Muleba, ambaye alikuwa akikabiliwa na tatizo la kuvimba mguu na alihitaji fedha kwa ajili ya upasuaji.

Stewart Onesmo alisema aliomba msaada wa shilingi laki sita, lakini baada ya kufikishiwa ombi hilo, Mkurugenzi wa Wenfurebe Foundation aliamua kumsaidia zaidi kwa kumpatia shilingi milioni moja ili aweze kugharamia matibabu na upasuaji wa mguu.

Mnufaika mwingine ni Angelina Dauson, mkazi wa Kitongoji cha Kanone, Kijiji cha Kasheno, Kata ya Magata/Karutanga, ambaye mtoto wake anaumwa ugonjwa wa moyo na anahitaji kufanyiwa upasuaji.

Familia hiyo imepatiwa shilingi milioni tatu kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo, msaada ambao umeondoa sehemu kubwa ya mzigo wa kifedha uliokuwa ukiikabili familia hiyo.

Familia hizo, zilizopata.msaada huo wamesema kuwa hari hiyo imerejesha matumaini katika kipindi ambacho walikuwa wameanza kukata tamaa kutokana na changamoto za kiafya na maisha. 

Baadhi yao walieleza kuwa pamoja na matatizo ya afya, wamekuwa wakikabiliwa pia na changamoto mbalimbali ikiwemo kutengwa na wenza wao, hali iliyowafanya kuishi katika mazingira magumu na kupoteza matumaini ya maisha.

Akizungumza kuhusu msaada huo, mwakilishi wa Wenfurebe Foundation, Suleiman Adam, amesema taasisi hiyo ilipokea taarifa kuhusu hali za familia hizo na Mkurugenzi wa taasisi, Simon Patrick Wenfurebe, akaamua kuingilia kati kwa kutoa fedha za matibabu.

Amesema lengo la taasisi hiyo ni kuhakikisha watu wanaokabiliwa na mazingira magumu hawabaki peke yao, bali wanapata msaada unaoweza kurejesha matumaini na kuwapa nguvu ya kuendelea kupambana na changamoto za maisha.

Wenfurebe Foundation imesema imepanga kutenga shilingi milioni 100 kwa mwaka wa 2026/2027 kwa ajili ya kusaidia familia zenye uhitaji wa matibabu, hususan zile ambazo zimekuwa zikifanya michango ili kugharamia matibabu. 






Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top