Waziri Mkumbo Afungua Wiki ya Ubunifu Tanzania 2026

0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), amefungua rasmi Wiki ya Ubunifu Tanzania (Innovation Week Tanzania 2026 IWTz2026)

Akizungumza katika ufunguzi huo uliofanyika Tarehe 31 Agosti 2026 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Mhe. Waziri Mkumbo ametoa wito hasa kwa vijana wa Tanzania kuachana na mazoea ya kawaida na kuwekeza nguvu kwenye ubunifu na teknolojia ili kuelekea utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050! 

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Anayeshughulikia Mambo ya Afrika Mashariki Mhe. James Kinyasi Millya (Mb) ameisihi Sekta Binafsi kufanya kazi kwa bidii na ubunifu wa hali ya juu ili kukuza uchumi wa nchi na kufanikisha ndoto ya Dira ya Uchumi 2050

✍🏻wizara ya mambo ya nje











Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top