Tanzania Yatoa Msaada wa Tani 52 za Bidhaa za Afya kwa DRC Kukabiliana na Ebola

0


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeikabidhi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tani 52 za dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 220, sawa na takribani dola 88,000 za Kimarekani, kusaidia mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Msaada huo umekabidhiwa  Septemba 5, 2026 jijini Kinshasa na Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Florence George Samizi, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Bidhaa zilizotolewa zinajumuisha dawa, vifaa kinga kwa ajili ya wahudumu wa afya, vifaa tiba na mahitaji mengine kwa ajili ya kuimarisha huduma kwa wagonjwa na kukatiza mnyororo wa maambukizi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Samizi amesema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Tanzania katika majukwaa mbalimbali ya afya ikiwemo Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola uliofanyika kwa njia ya mtandao 16 Juni, 2026, katika kukabiliana na majanga ya kiafya ambayo hayatambui mipaka.

Kwa upande wake Katibu wa Waziri wa Afya wa DRC, Dkt. Romain Muboyayi, ameishukuru Tanzania kwa msaada huo, akisema umeonesha undugu, urafiki na ushirikiano imara uliopo kati ya nchi hizo mbili chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Rais Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo.





Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top