Je Wajua, Kuchapisha Taarifa au Data za Uongo, Zinazopotosha na Zisizo Sahihi ni Kosa Kisheria?

0

 


#MusomaCheck Je, wajua kuwa kuchapisha taarifa au data uongo zinazopotosha na na zisizo sahihi mtandaoni ni kosa kisheria?

Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kinahusu uchapishaji wa taarifa za uongo na kinaeleza adhabu kwa mtu atakayepatika na hatia.

Sheria inaeleza kuwa  “Mtu atakayechapisha taarifa au data katika picha, maandishi, alama au katika namna nyingine yoyote katika mfumo wa kompyuta, akijua kwamba taarifa au data ni za uongo, zinapotosha, zisizo sahihi, na kwa lengo la kudhalilisha, kutishia, kutusi au kwa naamna nyingine kudanganya umma au kuchochea utendaji wa kosa, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.”

Unapopokea taarifa mtandaoni jiulize:

1. Chanzo chake ni kipi?
2. Taarifa hii imethibitishwa?
3. Ina ushahidi?
4. Taarifa hii inaweza kumpotosha au kumdhuru mtu mwingine?
5. Nina uhakika wa kutosha kuisambaza?

#Usisambaze kwa sababu tu imeletwa na rafiki.
#Usiamini kwa sababu tu inaonekana kwenye picha.
#Usisambaze kwa sababu tu watu wengi wameisambaza.

Unachotakiwa kufanya,Fikiri kabla ya kuchapisha na Chunguza kabla ya kusambaza.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top