Mbunge Nsekela Ahaidi Kutatua Changamoto ya Maji Kimuli

0


Na Angela Sebastian 

Kyerwa : Mbunge wa Kyerwa, Khalid Nsekela, ameahidi kushirikiana na Halmashauri pamoja na wadau wa elimu kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama katika Shule ya Sekondari Kimuli, ili kuwawezesha wanafunzi kutumia muda mwingi kujisomea badala ya kutembea hadi saa nne kufuata maji.

Ahadi hiyo imekuja wakati wa afla ya utoaji tuzo kwa walimu na shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kidato cha sita 2026, licha ya shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma, ambapo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2026 ilishika nafasi ya kwanza wilayani,ya kwanza kwa shule za Serikali kimkoa na ya pili kimkoa kwa shule zote.

Kimuli inakabiliwa pia na changamoto ya ukosefu wa ofisi za walimu na mabweni, hali inayowalazimu baadhi ya wanafunzi kulala katika vyumba vya madarasa visivyo na madirisha lakini wanafanya vizuri katika masomo yao.

Kwa niaba ya Mbunge,   Nekmia Nguma Katibu wa Mbunge-Kitengo cha Mahusiano, amesema Nsekela amewapongeza wanafunzi na walimu kwa matokeo hayo, huku akiahidi pia kusaidia walimu 40 waliopanga kutembelea Mulongo kwa ajili ya utalii wa ndani.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kyerwa, James John, amesema changamoto ya maji imewasilishwa ofisini kwake na imepewa kipaumbele kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.






Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top