DCEA Yatoa Elimu Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya Kwa Wanafunzi Chuo cha Magereza Kiwira

0


 Wanafunzi 1,561 wa Kozi Na. 33/2025/2026 katika Chuo cha Magereza Kiwira, Tukuyu, mkoani Mbeya, wamepatiwa elimu kuhusu tatizo la dawa za kulevya kutoka kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Katika programu hiyo, askari wanafunzi hao wamepatiwa uelewa kuhusu aina na madhara ya dawa za kulevya, sababu na vihatarishi vinavyochangia matumizi, pamoja na viashiria vya matumizi ya dawa hizo.

Aidha, wameelimishwa kuhusu nafasi na wajibu wa askari wa magereza katika kuzuia matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya katika mazingira ya kazi na jamii.

Vilevile, wamepatiwa elimu kuhusu namna ya kuwashughulikia watu wenye changamoto za matumizi ya dawa za kulevya kwa kuzingatia utu, usalama na haki zao, pamoja na umuhimu wa kuwaunganisha wanaohitaji msaada na huduma stahiki za matibabu, unasihi, urekebishaji na urejeshwaji katika jamii.

DCEA inaendelea kushirikiana na taasisi za Serikali katika kujenga uwezo wa watumishi na wadau mbalimbali ili kuimarisha juhudi za kuzuia matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.

✍🏻DCEA








Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top