.
👉Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zabuni.
👉Sheria ya Manunuzi ya Umma (Public Procurement Act) na kanuni zake, hasa kupitia marekebisho yaliyofanywa kuanzia mwaka 2016 kuzingatiwa.
ZABUNI za Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana kupitia mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST) imetangaza fursa za kipekee zinazolenga kuyainua makundi maalum kiuchumi. Mpango huu unatoa kipaumbele kwa kutenga 30% ya zabuni zote za Serikali maalum kwa ajili ya makundi haya, hatua ambayo inaenda kubadilisha kabisa mwelekeo wa kiuchumi kwa vijana na taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Edith Semtengu, amesema ili kuhakikisha usawa na ushirikishwaji mpana, asilimia hizi zimegawanywa kwa usawa kwenye makundi matatu muhimu, ambapo Wanawake (10%), Vijana (10%) na Watu Wenye Ulemavu (10%).
“Kwa hivyo upatikanaji wa zabuni hizi kupitia mfumo wa NEST sio tu utaleta usawa, bali unajenga msingi imara wa kiuchumi kwa vijana kupitia yafuatayo; Uwazi na Usawa (Haki Sawa kwa Wote), Upatikanaji wa Mitaji ya Uhakika, Kutengeneza Ajira Mpya Mitaani, Kuhamasisha Urasimishaji wa Biashara na Kukuza Ujuzi na Uzoefu” ameyasema hayo Bi. Semtengu.
Sanjari na hayo, Mkufunzi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Emmanuel Simbeye, amesisitiza ya kuwa wakati ni sasa! Vijana, wanawake, na watu mwenye ulemavu wenye ndoto za kiuchumi wanapaswa kuchangamkia fursa hii. Wajisajili katika mfumo wa NEST, wakamilishe nyaraka za makampuni au vikundi vyao, na waanze kuomba tenda hizi. Huu ni wakati wa kuacha kuwa watazamaji na kugeuka kuwa washiriki wakuu katika ujenzi wa uchumi wako na Taifa.
✍️maendeleo ya vijana


