Mradi wa Lishe Yangu Wazinduliwa Rasmi

0


Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI, na Shirika Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), imezindua rasmi mradi mkubwa wa Kuboresha lishe ya Mama Mjamzito awamu ya pili ujulikanao kama “LISHE YANGU” utakaotekelezwa katika mikoa ya Songwe, Njombe, Mbeya na Dodoma.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mradi huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbarak Alhaj Batenga,  amesema  mradi huo unalenga kuimarisha mifumo ya utoaji huduma bora na kusaidia utekelezaji wa afua za lishe kwa mama mjamzito 

Batenga amesema  mradi huu unaenda kutoa ushaidi wa kisayansi na kuisaidia  serikali kuboresha huduma za lishe kwa wanawake wajawazito nchini.

Akiwasilisha salama kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Bw. Luitfrid Nnaly, amesema watasimamia lkikamilifu  utekelezaji wa mradi huu, kuanzia ngazi ya Mkoa hadi chini kwani  umejikita kuendeleza jitihada za Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha lishe, afya na ustawi wa wanawake wajawazito na kumpa kila mtoto mwanzo bora wa Maisha.

Naye Bi Joyce Ngegba ambaye amemwakilishi Mkuu wa Masuala  ya Lishe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF),ameipongeza Serikali kwa uongozi na dhamira yake endelevu ya kuimarisha lishe ya Watoto wajawazito.

“mradi wa LISHE YANGU unatoa fursa ya kuimarisha mifumo ya utoaji huduma bora na kusaidia utekelezaji wa afua za lishe kwa mama mjamzito na sisi UNICEF  tunaamini kuwa kuwekeza katika lishe ya wanawake ni moja ya uwekezaji muhimu zaidi kwa ajili ya uhai, ukuaji na maendeleo ya Watoto.

Kwa upande wake  Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lisha Tanzania Dkt. Germana Leyna, amesema mradi huu utaenda kufahamu kwa kina tatizo la lishe hususan kwa akina mama wajawazito sambamba na kubaini visababishi vyake na kupitia mradi huu  unaenda kuboresha lishe ya mama mjamzito ikiwemo kwenye utoaji wa elimu na unasihi na kwenye matumizi ya virutubishi mchanganyiko.

✍️TFNC











Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top