NIDA Yatoa Tahadhari kwa Wananchi Kagera Kuepuka Jumbe za Wezi wa Mitandaoni

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba : Afisa habari wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) makao makuu Alfan Mlacha amewashauri wananchi wa mkoa wa Kagera kupuuza jumbe ambazo zimekuwa zikitumwa na wezi wa mitandaoni zikiwataka  kulasimisha laini zao.

Mlacha ameyasema hayo leo katika maonyesho ya elimu ya juu kupitia bodi ya mikopo (HESLB) yanayoendelea katika viwanja vya soko kuu mjini Bukoba ambapo amesema kuwa, kuna watu wanaojihusisha na utapeli wa kutumia simu za mkononi ambao wamekuwa wakituma jumbe za kawaida wakidai wao ni Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kuwa jumbe hizo zipuuzwe.

Mlacha ameeleza kuwa, jumbe hizo zinazotumwa kupitia simu za mkononi za watu binafsi zinapaswa zipuuzwe, kama kuna mtu ana jambo lolote kuhusu vitambuliaho vya taifa (NIDA) awasiliane na kituo chao cha huduma kwa wateja kupitia namba 0232210500.

“Ukiona watu wanadukua kitu fulani au huduma fulani ujue huduma hiyo ni ya muhimu sana kwa jamii kwahiyo NIDA ni sehemu ya muhimu kwa wananchi  wasidanganyike na watu wenye nia ovu,pia mtu akikwazika kwa taarifa yoyote ambayo inahitaji maelekezo kuhusu NIDA mnashauriwa kufika ofisi za NIDA ili mpate maelekezo na kama mko mbali na mji tumia namba yetu ya mtoa huduma” amesema Mlacha

Wakati huo huo ametaja lengo la wao kuwepo katika maonesho hayo kuwa, wanafunzi wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu wanapata elimu kwao jinsi ya kujisajiri na kujiandikisha kwa maana ya kwamba wanapaswa kuwa na taarifa sahihi kama vile, cheti cha kuzaliwa kifanane na taarifa zao za NIDA pamoja na za wazazi.

Maonyesho hayo ya elimu ya juu yatafanyika kwa siku tano kuanzia Mei 26 hadi Mei 30, maka huu lengo likiwa ni kutoa elimu kwa vijana waweze kuepukana na utapeli ambao umekuwa ukifanya na baadhi ya watu ambao si waaminifu na hujifanya maafisa wa Serikali wakati ni matapeli.


Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top