Shirika la Ladies Joint Forum Latambulisha Mradi wa Paza Mwendo Misungwi

0


Shirika la Ladies Joint Forum Kwa kushirikiana na Kijiweni Production wameutambulisha mradi wa Paza Mwendo wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Akielezea lengo la mradi huo mkurugenzi wa Shirika LJF Fransisca Mboya amesema lengo ni kuwawezesha Wanawake kuiandaa Filamu za Makala bunifu zinazo wagusa Wanawake watengeneza Filamu na madereva Bajaji Wanawake.

"Tumeanza na wanawake sita kutoka Dar es Salaam na Mwanza hawa watapewa ujuzi wa kuandaa Makala zenye Ubunifu na Kwa kuanza wataanza kuandaa Makala zinazowahusu Wanawake madreva wa Bajaji ambao tuliwapata kupitia mradi wetu wa She drives to Change"alisema Mboya

Kwa upande wake mkurugenzi wa Kijiweni Production Amil Shivji amesema baada ya kuelezwa kuhusu mradi wa She drives to Change walivutiwa na kuja na wazo hilo la kuandaa Makala zinazoelezea Maisha ya Wanawake hao na kuona ni vema hata wazalishajii wa Makala hizi wawe pia Wanawake.

Awali akifungua warsha hiyo ya mafunzo Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Dr Shami Chrispin ameahidi kuwapatia mikopo Wanufaika wa mradi huo kupitia fedha za asilimia 10 ambazo hutolewa Kila Kila mwaka kwaajili ya Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu.

"Niwashukuru Ladies Joint Forum pamoja na Kiweni Production Kwa kuuleta mradi huu hapa kwetu Misungwi chochote mtakachohitaji naomba mtujulishe.

Shirika la Ladies Joint Forum Kwa Kushirikiana na Kijiweni Production wanaendedha Mradi huo wa Paza Mwendo kupitia mradi wa Vijana@Work na unatekelezwa na Goethe-Instute Tanzania Kwa kushirikiana na Culture and Development East Africa Kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.

Mradi huu wa Paza Mwendo unawakutanisha watengeneza Filamu wa kike na madereva Bajaji Wanawake kuunda Filamu za Makala bunifu zinazosimulia Maisha Yao ya Kila siku.





Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top