NEMC na THPS Wakutana kujadili ushirikiano katika masuala ya afya ya jamii ya mazingira

0


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) wamefanya kikao cha pamoja kuhusu ushirikiano katika masuala ya usimamizi wa mazingira na afya ya jamii tarehe 10 Machi 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, pande zote mbili zimejadiliana na kukubaliana kushirikiana katika kujengea wadau uelewa kuhusu afya ya binadamu na mazingira, kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha tafiti kuhusu uhusiano kati ya mazingira na afya ya binadamu, pamoja na kuboresha usimamizi endelevu wa taka zitokanazo na huduma za afya.

Ushirikiano huu unalenga kuunga mkono juhudi za Taifa katika kulinda mazingira, kuboresha afya ya jamii na kuchochea maendeleo endelevu sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayosisitiza umuhimu wa mazingira salama na jamii yenye afya kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

✍️nemc

 

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top