Dkt. Godlove Isdory ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Primelife Heath ya jijini Dar es Salaam, amebainisha hayo wakati akiwasilisha mada jinsi pombe ba vileo zinavyoathiri afya za vijana katika warsha ya siku mbili kwa asasi za kiraia na mashirika ya kijamii mkoani Mara iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Integrating Capacity and Community Advancement Organization (ICCAO) ili kusaidia katika utekelezaji wa mradi wa "Ulevi Sio Dili" unaolenga kupunguza athari za ulevi kwa vijana katika wilaya za Musoma, Butiama na Bunda mkoani Mara pamoja na mikoa mingine minne nchini.
Dkt.Isdory amesema mradi huo unalenga usaidia kuzuia ukiukwaji wa haki na madhara yatokanayo na matumizi ya vilevi ambavyo ni pombe na madawa ili kuwawezesha vijana kuboresha Hali ya uchumi pamoja na afya katika jamiu.
Amesema kuwa ongezeko la matumizi ya pombe haramu na dawa za kulevya miongoni mwa vijana limesababisha kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza, kushuka kwa uzalishaji na kudorora kwa hali ya kiuchumi na kiafya, jambo linaloweza kuzaa kizazi cha watu tegemezi katika miaka ijayo.
Ameongeza kuwa, kwa mujibu wa takwimu za Idara ya Maendeleo ya Jamii, asilimia 76.5 ya vijana wa Kitanzania wako katika hatari ya kuathirika na matumizi ya pombe na dawa za kulevya, hali inayoweza kuathiri kwa kiasi kikubwa nguvu kazi ya taifa.
Aidha amewataka wazazi na walezi kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao, kuwapatia elimu sahihi kuhusu madhara ya ulevi na kufuatilia mienendo yao ili kuwaepusha kuingia katika makundi hatarishi.
“Ni wakati sasa kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushirikiana katika malezi bora ya vijana wetu ili kulinda kizazi cha sasa na kijacho,
Hivi sasa vijana wengi wanekua wakipata magonjwa yatokanayo na unywaji pombe na matumizi ya dawa za kulevya yanayoathiri damu, Figo psmoja na ini hali inayosababisha pia kuwepo na ongezeko la vijana chini ya miaka 40 kufika hosipitali kufuata huduma ya kusafisha Figo" Amesema Dkt.Isdory.
Awali akiongea wakati wa kutambulisha mradi huo kwa asasi za kiraia na mashirika yasio ya kiserikali mkoani Mara, msimamizi wa miradi kutoka shirika lisilo la kiserikali la Integrating Capacity And Community Advancement Organization(ICCAO) Mary Mrindoko amesema kuwa mradi huo katika awamu ya kwanza ulianza mwaka 2023 hadi mwaka 2025 na sasa unatekelezwa katika awamu ya pili lengo ikiwa ni kupunguza athari za matumizi ya Pombe kupita kiasi kwa asilimia 5 kwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 35 katika mkoa wa Mara
Amesema pia mradi huo unaotekelezwa kwa ufadhili wa IOGT.NTO.MOVEMENT la nchini Sweden, umelenga kufanya kazi na wanawake vijana, wasichana balehe na watoto huku likilenga pua kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za kiraia na maendeleo ili kutumia uwezo wa idafi kubwa ya vijana wa Tanzania kwa ajili ya ukuaju na maendeleo ya nchi.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wakiongea wakati wa kuchangia mada hiyo wamesema pia Kuna haja ya kwa serikali na wadau wa maendeleo kufanya mapito ya Sheria na Sera ili kusaidia kulinda afya za watoto na vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa
Simon Chupa kutoka shirika la Community Hope Raising Foundation(CORAF) ni Moja ya washiriki katika warsha hiyo ,amesema katika jitihada za mapambano ya ulevi na madawa ya kulevya ni vyema pia inahitajika kufanya mapitio katika Sheria ya ulevi kwa watoto.
" Mfano sheria inaeleza wazi kuwa ni makosa kwa mtoto kukaa katika maeneo ya sterehe ambapo kunapatikana vilevi baada ya saa kumi na mbili za jioni na endapo mtu atakamatwa yupo na mtoto baada ya muda huo anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.
Robinson Wangaso kutoka taasisi ya Tanzania Community Care Organization, amesema vijana wengi wameendelea kuathirika na Pombe na Vilevi kutokana na huduma hiyo Kwa sasa kupatikana kila sehemu na kwa urahisi tofauti na ilivyokua huko nyuma ambapo pombe zilikua zinapatikana maeneo ya starehe tofauti na sasa inavyopatikana hata katika madukani.
" Kwa sasa pombe zinapatikana katika maduka kila sehemu na hata kama ni mtoto au kijana ambaye yupo chini ya miaka 18 akienda kununua hakuna mtu anayehoji na unaluta wengine hawana uelewa juu ya madhara ya vitu hivi" Amesema Robinson
Naye Debora Sandhu kutoka shirika la Victory Hope Foundation Organization Tanzania(VIHOFOTA) amesema vijana wengi Kwa Sasa wanajihusisha na vitendo vya ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na mmomonyoko wa maadili kwa vijana kutowaheshimu wazazi na walezi.
" Vijana wengi hivi sasa hawana heshima kwa wazazi au walezi Kila wanachoambiwa Hawaii na wanajiona wao ndio wanajua vitu vingi kuliko wazazi wao.
Unakuta wazazi wanamwambia kijana hapa nyumbani unatakiwa kurudi mwisho saa kumi na mbili au usitumie vilevi au madawa vina madhara lskini unaposema hivyo ndio kama unakua unachochea" Amesema Debora
Shirika la ICCAO linatekeleza mradi huo ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha vijana na jamii kuhusu elimu Rika Kwa Rika, uhamasishaji mashuleni kupitia mijadala, sanaa klabu, michezo na kampeni za kuhamasisha maisha yasiyo na pombe, vipindi vya redio podcast na midahalo ya kijamii.
Mkatakati wa pili ni uwezeshaji vijana kwa kuwapatia mafunzo ya stadi za maisha na Uongozi, mafunzo ya ujasiliamali na vitendea kazi vya kuanzia, njia mbadala chanya za kiuchumi badala ya shughuli zinazohusiana na pombe.
ICCAO pia katika mkakati wake wa utekelezaji inalenga kuimarisha asasi za kiraia kwa kuwajengea uwezo asasi zinazoongozwa na vijana na wanawake, kuunda mtandao wa vijana na wanawake wa kuzuia madhara ya pombe na ukatili wa kijinsia pamoja na majukwaaya kujifunza kwa pamoja na kufanya utetezi.
![]() |

















