Tanzania yajipanga kuwa mwenyeji mkutano wa Hortilogistica Africa Novemba 2026

0


Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeeleza kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kikanda wa Sekta ya Mbogamboga na Matunda (Hortilogistica Africa) mwezi Novemba 2026, mkoani Arusha.

Mkutano huo unalenga kukutanisha wadau mbalimbali kujadili, kubadilishana uzoefu na kunadi fursa za mnyororo wa thamani katika kilimo zikiwemo uwekezaji, utalii, biashara na uchukuzi.  Jukwaa hilo litatoa nafasi kwa Tanzania kama kitovu cha uzalishaji wa mazao ya mbogamboga na matunda barani Afrika(Tanzania as Africa’s horticulture hub).  

Akizungumza wakati wa kikao kazi cha maandalizi ya awali, Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amemshukuru Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa utayari wake wa kutoa ushirikiano katika kuhakikisha maandalizi ya Mkutano huo yanaleta tija siyo tu katika Sekta ya Kilimo, bali pia kupanua wigo wa fursa za kibiashara na uwekezaji kwa sekta nyingine nchini. 

Kwa upande wake, Prof. Kitila amependekeza kuwa Mkutano tarajiwa uzingatie kukuza uwekezaji katika uzalishaji wa mazao, masoko na ushirikishwaji wa sekta mtambuka ili kuleta maendeleo nchini. 

Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli amesema kuwa uratibu wa pamoja kati ya Wizara ya Kilimo na TAHA ni utekelezaji wa dira ya Serikali ya kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuchochea maendeleo nchini.  Ameongeza kuwa TAHA ni mdau muhimu ambapo ushirikiano wake ni wa muda mrefu katika matukio mbalimbali ya Sekta ya Kilimo, huku akitplea mfano Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane. 

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Dkt. Fred Msemwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Uwekezaji; wakiwemo wawakilishi kutoka Asasi Kilele ya Sekta Binafsi inayoendeleza na kukuza sekta ya horticulture nchini (TAHA); na Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA).

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top