Tanzania na Ireland Zaimarisha Ushirikiano Uwezeshaji Wanawake na Usawa wa Kijinsia

0


Na Jackline Minja WMJJWM- Dodoma

Imeelezwa kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland katika utekelezaji wa Agenda ya Kizazi chenye usawa itaimarisha Uwezeshaji wa Wanawake na usawa wa kijinsia nchini.

Hayo yamebainika jijini Dodoma tarehe 03 Februari,2026 wakati wa katika kikao cha heshima kilichowakutanisha Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Dkt. Gwajima ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kama nguzo muhimu za maendeleo jumuishi na endelevu, kwa kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya mwaka 2023, Serikali inaendelea kuhakikisha masuala ya jinsia yanajumuishwa kikamilifu katika sera, mipango na bajeti za sekta zote. 

Aidha, Waziri Dkt. Gwajima amebainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinazotekeleza Jukwaa la Kimataifa la Usawa wa Kijinsia (Generation Equality), ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni Kinara wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi kwa Wanawake.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa ahadi hizo unahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na wadau wa maendeleo, akitaja mchango wa Serikali ya Ireland kuwa ni wa muhimu na wenye matokeo chanya kwa wanawake na wasichana nchini. 

Kwa upande wake, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan, amesema Serikali ya Ireland itaendelea kushirikiana na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kukuza usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake na kupambana na ukatili wa kijinsia. 

Amesisitiza kuwa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania na wadau wengine imechangia kuboresha maisha ya wanawake na wasichana, na kwamba Ireland iko tayari kuendeleza na kuimarisha ushirikiano huo kwa maendeleo endelevu ya jamii.

chanzo: maendeleo ya jsmii








Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top