Tafiti Zatajwa Kuwa Nguzo Muhimu Katika Kukabiliana na Magonjwa ya Milipuko

0


Na WAF - Dar es Salaam 

Imeelezwa kuwa tafiti ni nguzo kuu katika kuimarisha maandalizi na uwezo wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko nchini pamoja na kutoa ushahidi muhimu unaoongoza maamuzi ya sera, miongozo na mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, kusaidia ugunduzi wa mapema, ufuatiliaji wa magonjwa na uendelezaji wa vipimo, chanjo na tiba.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe leo Februari 11, 2026 wakati wa kikao na Taasisi ya Utafiti ya Jeshi la Marekani 'Walter Reed Army Institute of Research' (WRAIR) kilichofanyika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam. 

"Tanzania imeweka vipaumbele maalum vya kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na mwitikio wa magonjwa (IDSR), kupanua uwezo wa maabara ikiwemo ufuatiliaji wa vinasaba, kuimarisha mifumo ya afya ya kidijitali na matumizi ya takwimu ili kufanya maamuzi," amesema Dkt. Magembel.

Amesema, ameiomba Taasisi hiyo kufanya kazi kwa karibu na Hospitali ya Kibong'oto na Maabara ya Taifa kugundua na kufuatilia magonjwa kwa kuwa zimepata ithibati ya Kimataifa.   

Aidha, Dkt. Magembe amesema kuwa Serikali inaona fursa kubwa ya kuendeleza ushirikiano wa kimkakati na Taasisi ya Utafiti ya Jeshi la Marekani ya Walter Reed (WRAIR), hususan katika mifumo ya tahadhari ya mapema, ufuatiliaji na uchambuzi wa takwimu, uundaji wa mifano ya utabiri, uhamishaji wa teknolojia na uimarishaji wa uwezo wa tafiti za ndani kupitia taasisi kama NIMR na usugu wa vimelea dhidi ya dawa (AMR).   

Kwa upande wake Kanali Brianna Perata ambae ni Kamanda wa Taasisi ya Utafiti wa Jeshi la Marekani ameahidi kuwa Taasisi hiyo ya Kijeshi ya Marekani itaendeleza ushirikiano na Tanzania hasa katika tafiti mbalimbali ili kuboresha sekta ya afya nchini na kuomba kuendelea kupewa ushiriliano na Tanzania.

Maeneo yaliyopendekezwa kwa ushirikiano wa haraka katika kikao hicho ni pamoja na kukusanya, kuunganisha na kuchambua takwimu za usugu wa vimelea dhidi ya dawa (AMR), kuimarisha uunganishaji wa takwimu za afya ya kidijitali na maabara katika mfumo mmoja wa kitaifa, kuimarisha uwezo wa maabara za kikanda hususan katika maeneo ya mipakani.

chanzo: wizara ya afya










Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top