Serikali Yaweka Mkazo Matumizi Sahihi na Endelevu ya Kondomu Kulinda Afya ya Jamii

0


Na WAF -Dodoma.

Serikali kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, magonjwa ya ngono na homa ya ini (NASHCoP) kwa kushirikiana na wadau, imeendelea kusambaza kondomu kwa wingi bila malipo katika vituo vya kutolea huduma za afya, ngazi ya jamii na maeneo ya kazi, hususan maeneo yenye makundi yaliyo hatarini zaidi ya kuambukizwa VVU.

Akizungumza kwa niamba ya Mganga Mkuu wa Serikali leo 13 Februari, 2026 Dkt.Boniface Silvan wakati wa maadhimisho ya Kondomu duniani yanayofanyika ukumbi wa Nyerere Square jijini Dodoma amesema Serikali imeendelea kusambaza kondomu kwa wingi bila malipo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, ngazi ya jamii na maeneo ya kazi, hususan katika maeneo yenye makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU.

“ Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2025, jumla ya kondomu za kiume 72,875,900 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 6.93 zilisambazwa bila malipo, pamoja na kondomu za kike 180,500 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 284. “amesema Dkt.Silvan

Pia Dkt.Silvan alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuimarisha utoaji wa elimu ya kinga na tiba, sambamba na kuhimiza maadili mema kwa vijana ili waweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya zao na kujikinga dhidi ya maambukizi.

“kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Jipende, Jilinde, Tumia Kondomu,” alisema ujumbe huo unalenga kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa kuthamini afya zao kwa kuchukua hatua za makusudi za kujikinga dhidi ya VVU, magonjwa ya zinaa, homa ya ini na mimba zisizotarajiwa.”

Aidha ,Dkt.Silvan aliwashukuru wadau mbalimbali wa maendeleo kwa mchango wao katika mapambano dhidi ya UKIMWI, wakiwemo World Health Organization (WHO), United Nations Population Fund (UNFPA), Global Fund, Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS), UNICEF, International Labour Organization (ILO), United States Agency for International Development (USAID), President's Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR), Centers for Disease Control and Prevention (CDC), UN Women pamoja na wadau wengine wa utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI nchini.


Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top