Serikali Yawaita Wananchi Kyerwa Kuchukua Vitambulisho vya NIDA

0


 Na Angela Sebastian 

Kyerwa :Serikali wilayani Kyerwa mkoani Kagera imewataka wananchi ambao hawajachukua vitambulisho vyao vya NIDA kuhakikisha wanavichukua ili kuondokana na malalamiko yasiyo ya lazima.

Mkuu wa Wilaya hiyo Zaituni Msofe amesema kuwa  wananchi wengi hawaja chukua vitambulisho vyao, vipo tuu katika ofisi za NIDA na jambo la kushangaza wananchi hawaendi kuvichukua  lakini wanaendelea kulalamika mitaani kuwa hawapati vitambulisho vyao.

Akiongea na Madiwani wakati wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za halmashauri kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026,Msofe amesema kuwa kwasasa Serikali imerahisisha upatikanaji wa vitambulisho lakini hawaelewi kwanini wananchi wameshindwa au wanagoma kuvichukua na kuongeza kuwa kuna wakati walitangaziwa kabisa kuwa watavipeleka katika kila ofisi za Kata husika lakini bado hawakufika na vitambulisho vyao vilirudishwa ofisini kwa mkuu wa Wilaya. 

"Kuna muda tulipeleka vitambulisho katika ofisi zenu za Kata kwa watendaji wa Kata lakini havikuchukuliwa na tukaamua virudishwe Sasa wananchi wambieni waache lawama vitambulisho vyao vipo na kwasasa Kyerwa tumepata mashine ya kuzalisha vitambulisho sio kama zamani tulipokuwa tunaenda katika wilaya jirani hivyo wambieni wananchi wenu wakafike ofisi za mkuu wa Wilaya wakavichukue vimerundikana"mesema Dc

Kadhalika amewasihi Madiwani hao kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mwananchi ambaye anastahili kitambulisho cha NIDA amejaza fomu kwa ajili ya kupigwa picha ili vyombo husika vianze mchakato ili kumpatia kitambulisho chake.







Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top