Serikali na WHO Kuendeleza Mikakati ya Kukabili Majanga ya Dharura

0


Na WAF, Dodoma 

Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) Idara ya Dharula na Maafa, pamoja na wadau kutoka taasisi za serikali na binafsi wamejiweke afua za tathmini ya athari za kiafya zitokanazo na majanga ya dharula katika mkoa wa Dodoma. 

Wakati wa kikao, washiriki wamejadili kwa kina athari za kiafya zinazotokana na majanga kama mafuriko, ukame, ajali za barabarani, milipuko ya magonjwa pamoja na majanga ya moto, huku mjadala ukiwa umejikita zaidi kuimarisha utayari wa sekta ya afya, uratibu wa wadau, pamoja na umuhimu wa elimu kwa jamii ili kupunguza athari kabla na baada ya janga kutokea. 

Akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi hicho Februari 13, 2026 jijini Dodoma, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Charles Mduma amesema kuwa kama ilivyo mikoa mingine, Dodoma pia inakumbwa na athari za kiafya zotokanazo na majanga ya dharula hususan magonjwa ya mlipuko yanayochagizwa na ongezeko la idadi kubwa ya watu. 

"Natambua sio matukio yote mliyoyaandaa yamepewa kipaumbele, hivyo nitoe wito kwa wataalam wetu wote kuendelea kujiandaa na kuweka utayari wa eneo hilo" amesema Bw. Mduma 

Ameongeza kuwa, kwa ngazi ya mkoa wa Dodoma Ofisi yake ndio inayoshughulika na uratibu wa dharura na maafa, hivyo kupitia kikao hicho mkoa umeyachukulia mafunzo hayo kwa uzito mkubwa, kwani yatasaidia kufanya mapitio ya mipango ya mkoa ili kukabiliana na dharura na kufanya uhakiki wa kifedha kwa kushirikiana na taasisi hizo hivyo kuweza kutekeleza mpango kazi ulioandaliwa na wataalam hao. 

Aidha, amewapongeza Wizara ya Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, WHO na washiriki hao kwa muda wote waliokaa pamoja na kuandaa mpango kazi huo, huku akisisitiza kuimarishwa kwa mafunzo endelevu kwa watoa huduma za dharura na kamati za kukabiliana na majanga. 

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu-Udhibiti wa Athari na Majanga kutoka Wizara ya Afya, Dkt James Heller amesema kuwa kupitia mpango kazi huo, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau, itaandaa kalenda maalum itakayowezesha kutambua nyakati hatarishi zitakazosaidia kuchukua hatua mapema na kuimarisha tahadhari katika mkoa wa Dodoma yaani 'Regional Risk Profile & Calendar 

Kwa upande wake muwezeshaji kutoka Shirika la Afya Duniani Dkt. Pili Kimanga amesema kuwa WHO inaendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kukabiliana na athari za kiafya zitokanazo na dharura kwa kuongeza uwezo wa uratibu na ushirikiano wa sekta mbalimbali, kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tahadhari mapema, kuunga mkono tathmini za Taifa na mikakati ya afya, kuimarisha utayari wa kikosi cha tiba za dharura, na kujenga uwezo wa kitaifa wa kukabiliana na dharura. 

Kupitia azimio hilo, washiriki wanatarajiwa kurejea katika maeneo yao wakiwa na dhamira ya kutekeleza kwa vitendo mikakati iliyokubaliwa.









Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top