Nsabi aishukuru serikali kwa kuwasaidia wawekezaji wa miradi ya mazingira nchini

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba: MKURUGENZI wa kiwanda cha kuchakata  taka za plastiki pamoja na mifuko cha Waste Plastic Enterprises kilichopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera   Justin Nsabi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa  kuwaunga mkono, kuwapa moyo na kutambua umuhimu wao wa kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kukusanya taka na kuzibadilisha kuwa fursa ya ajira kwa wananchi wa Bukoba.

Nsabi ametoa shukrani hizo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) festo Dugange alipotembelea kiwanda hicho na kukagua shughuli za uhifadhi wa mazingira zinazofanywa kiwandani hapo na kujionea akina mama na vijana zaidi ya 250 wakiendea na ukusanayaji uchambuzi na uchakataji wa taka ikiwa ni njia ya kijiingizia kipato na kutunza mazingira.

"Tunaishukuru Serikali ya Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutuunga mkono pindi tunapohitaji msaada wa Serikali hari iliyochochea maendeleo ya kiwanda hiki ambacho kimekuwa chachu ya kuzalisha ajira kwa wanawake na vijana"

"Wanaofanya kazi katika kiwanda hiki wanatoka sehemu mbalimbali za mkoa wa Kagera ambapo hujishuguulisha na ukusanyaji wa taka na kuleta kuuzia kiwanda na wengine wakichambua na kuchakata kisha kujipatia kipato"ameeleza Nsabi

Akisoma risala ya kiwanda kwa Naibu Waziri huyo, Mkurugenzi wa raslimali wa kiwanda hicho Mudy Jumanne amesema 

kuwa, kiwandani hapo wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mashine ya uzalishaji wa bidhaa za mwisho mara baada ya kuchakatwa kwa taka hizo.

Aliomba Serikali kukiwezesha kiwanda chao kupata mkopo wa masharti nafuu ili waweze  kufikia malengo yao ya kuchakata kwa ubora zaidi.

Kwa upande wa Naibu waziri Dugange  amesema, Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji ambao wanaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita kupitia shuguli zao za kubadili changamoto kuwa fursa kama ulivyofanya uongozi wa kiwanda hicho.

"Nawapongeza kiwanda chetu cha West Plastic hivyo hawa ni wadau wetu muhimu wanaosafisha mazingira yetu,kuleta ajira na kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla hii inaendana na sera ya Serikali ya kusafisha mazingira na ustawi wa mabadiliko ya tabia nchi hongereni kwa kazi nzuri"Naibu waziri Dugange 

Amesema kuwa, uwepo wa kiwanda hicho umeleta faida zaidi ya tatu kwa wakati mmoja kwa wananchi wa  Kagera na Taifa hivyo akashauri mkoa na Manispaa kuendelea kushirikiana na uongozi wa kiwanda na kuzitambua kwa wakati changamoto walizonazo  ili ziweze kufanyiwa kazi kwa sababu ni wadau muhimu kwa Serikali.

Ameeleza  kuwa, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan inaendelea kuthamini mchango unaotolewa na wawekezaji  katika Sekta binafsi hususani wanaojihusisha na Utunzaji na hifadhi wa mazingira, kwahiyo Serikali itaendelea kuboresha kwasababu ndiyo nia ya Rais wetu kuona wadau wanafanya kazi zao katika hari ya kuridhisha.

















Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top