Mawakili wa Serikali Watakiwa Kuimarisha Mbinu za Mawasiliano ya Kimkakati

0


Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel M. Maneno amewataka Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuimarisha mbinu za Mawasiliano ya Kimkakati ili kuongeza ufanisi katika kutetea maslahi ya umma na kulinda taswira ya serikali kisheria.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikalia, ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu kuhusiana na masuala ya Habari na Mawasiliano ya Kimkakati na Vyombo vya Habari yanayofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 10 hadi 11 Februari, 2026.

Aidha, Mhe. Maneno amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa Mawakili wa Serikali kwakuwa yatawasaidia Mawakili hao kuongeza weledi na uwezo wa kuwasiliana na makundi mbalimbali ya wadau kwa ufasaha.

“Wakili wa Serikali anatakiwa kuwa mwelewa wa mazingira ya mawasiliano na muhimu zaidi aweze kueleza masuala ya kisheria kwa lugha inayoeleweka na wananchi kwa wadau hususan wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali”. Amesema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali 

Katika Hatua nyingine, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amewataka kutumia ujuzi watakaoupata katika mafunzo hayo katika kuelimisha umma na wadau kuhusu sheria zinavyowiana na malengo ya Dira 2050.

“Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka kwakuwa ujuzi mtakaoupata hapa utakuwa ni nyenzo muhimu katika kuelimisha wananchi na wadau kuhusiana na maboresho mbalimbali ya Kisheria yanayoshabihiana na malengo ya Dira 2050”. Amesema Mhe. Maneno

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa BSM Washauri ambao ni waandaji wa mafunzo hayo, Bi. Edna Minja amesema kuwa mafunzo hayo ni mahususi katika kuwawezesha Mawakili wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwasiliana kwa ufanisi, kulinda na kutetea maslahi na hadhi ya Ofisi na kuimarisha Imani ya Wananchi katika utendaji wa Ofisi na Serikali kwa ujumla kupitia Mawasiliano ya Kimkakati.

Naye, Wakili wa Serikali, Bw. Carson Nkya ameushukuru uongozi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia Mawakili wa Serikali katika kuwasilisha taarifa mbalimbali za kisheria kwa umma na wadau katika njia nyepesi na yenye kueleweka zaidi.

Mafunzo ya Masuala ya Habari na Mawasiliano ya  Kimkakati na Vyombo vya Habari, yameratibiwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yanafanyika kwa siku mbili ambapo Mawakili wa Serikali watapata nafasi ya kujifunza mada mbalimbali, ikiwemo Mawasiliano ya Kimkakati, Mbinu za kukabiliana na migogoro ya kimaelezo (Crisis Management) na mahojiano ya ana kwa ana (interviews).

chanzo : ofisi ya mwanasheria mkuu. 

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top