Wakandarasi Wazawa Wasisitizwa Kukamilisha Miradi ya Umwagiliaji Kwa Ufanisi

0


Wakandarasi wazawa wanaotekeleza miradi ya umwagiliaji nchini wametakiwa kuhakikisha miradi hiyo inakamilishwa kwa ufanisi na kuepuka uzembe au kuchelewesha utekelezaji ambapo hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa.

Amesisitiza hayo Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) tarehe 8 Januari 2026 mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la Kasoli lililopo Kijiji cha Kasoli, Kata ya Kasoli. Bwawa hilo lina ujazo wa takribani mita za ujazo milioni 2.7 na linatarajiwa kuhudumia mashamba yenye ukubwa wa hekta 650.

Mhe. Silinde amesema kuwa uamuzi wa Serikali kuwapa wakandarasi wazawa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo ya umwagiliaji, unalenga kuwajengea uwezo na kukuza ujuzi wa ndani ili wazawa washiriki kikamilifu katika kujenga uchumi nchini. “Imani  hiyo lazima iendane na uwajibikaji, ubora wa kazi na ukamulishaji wa miradi kwa wakati uliopangwa.  Ni wajibu wenu kuhakikisha miradi hii inaleta matokeo chanya na yenye tija kwa wakulima, kinyume chake hatua zitachukuliwa,” amesema Mhe. Silinde.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa “hili ni kati ya mabwawa makubwa yenye uwekezaji mkubwa katika Wilaya yetu ya Bariadi na ni nitegemeo kubwa kwa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji,” amesema Mhe. Macha.

Ujenzi wa Bwawa la Kasoli umefikia asilimia 90.2 na kukamilika kwake kunatarajiwa kunufaisha zaidi ya wakulima 15,000, hususan wanaojishughulisha na uzalishaji wa mazao ya Mpunga, Mahindi na Mbogamboga, hivyo kuongeza tija ya uzalishaji, kipato cha wakulima na usalama wa chakula katika Mkoa wa Simiyu na maeneo jirani.

Chanxo: wizara ya kilimo

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top