Ghati Msamba- Musoma
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) 24 Januari, 2026 imeanza ziara katika Mkoa wa Mara kwa ajili ya kuhamasisha uwekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Mara na kutembelea miradi ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba na Hoteli katika Manispaa ya Musoma.
Mwenyekiti wa bodi ya TISEZA amewataka watanzania kujisajili na Taasisi yaTISEZA na kuwataka vijana kuunda vikundi Ili kukuza masoko ya ndani na kutumia rasirimali zilizopo kupata fursa .
Lengo la kufanya ziara ni kutoa elimu Ili kuboshara na kuhamasisha uwekezaji wa kiuchumi Kwa watanzania watambue fursa zinazotolewa na TIZEZA
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya TISEZA Balozi Dk. Aziz Mlima amesema wapo katika Mkoa wa Mara kuendelea na kampeni maalum ya kuhamasisha katika fursa mbalimbali zilizopo katika Mikoa na Mara ni Mkoa wa pili baada ya kampeni hiyo kuzinduliwa rasmi katika Mkoa wa Geita hivi karibuni.
“Ninashukuru hapa (kwenye eneo la ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba) ninaona Serikali imehamasisha wadau wengi kuwekeza na taasisi za kifedha zimewaunga mkono na kwa kuwapa mikopo ya kufanikisha miradi yao” amesema Balozi Mlima.
Balozi Mlima amesema Kampeni hii inalengo kubadili fikra na mtazamo uliopo miungoni mwa watanzania kuwa uwekezaji ni mahususi kwa ajili ya raia na makampuni ya kigeni na kuwahamasisha mwamko wa wananchi kuwekeza na kuongeza idadi ya wawekezaji wa ndani katika sekta mbalimbali.
Balozi Mlima amesema Kampeni hii inawalenga makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo vijana, wajasiriamali wadogo na wakati, wafanyabiashara, waandishi wa habari na Maafisa wanaosimamia Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zote hapa nchini.
Balozi Mlima amesema kampeni hiyo itaanzisha madawati ya uwekezaji katika mikoa na Halmashauri na kuwataka waandishi wa habari kuwa mabalozi wa kufanikisha kampeni hiyo kwa kuandika kwa usahihi taarifa zinazotolewa kuhusiana na kampeni hiyo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Uhamasishaji Uwekezaji TISEZA Ndugu Geore Mukono amesema kuwa kampeni hiyo itaonyesha fursa mbalimbali zilizopo katika mikoa, taratibu za usajili wa miradi ya uwekezaji kwa lengo la kupata vyeti vya uwekezaji na leseni katika maeneo maalum ya kiuchumi, vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi vinavyotolewa kwa wawekezaji hapa nchini.
Mukono amesema wawekezaji watakaojisajiri watakapa unafuu wa ushuru wa forodha hadi asilimia 100 na msamaha wa kodi hadi asilimia 75 katika vifaa vinavyotumika katika uwekezaji baada ya mradi husika kusajiliwa.
Mukono ametolea mfano wawekezaji katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba wanaweza kupata msamaha wa kodi hadi asilimia 75 katika ununuzi wa maboti, injini, ndoano, magari ya kusafirishia samaki, vizimba, neti na kadhalika.
Kwa upande wake, Mwekezaji wa Hoteli mpya katika Manispaa ya Musoma Dkt. Felix Kivuyo amesema tangu amepata wazo la kufanya uwekezaji amepata ushirikiano kutoka kwa viongozi na watendaji wa Serikali na taasisi za kifedha ambazo zimemsaidia kutekeleza ndoto yake.
“Katika uwekezaji huu, nimefanikiwa kukutana na viongozi na watendaji mbalimbali ambao ushirikiano mkubwa na nimefanikiwa kupata mkopo kutoka benki za CRDB na NMB” amesema Dkt. Kivuyo.
Dk. Kivuyo amesema awali alikuwa mtumishi kwa sasa amestaafu na alianza s katika mradi huo mwaka 2022 na kwa sasa wapo katika hatua za ukamilishaji na hoteli hiyo itakuwa na v3èyumba vya kulala 21, ukumbi wa mikutano, mgahawa, bar na sehemu ya nje na inategemea kuajiri watumishi wakudumu 36 na watumishi wa muda 54.
Dk. Kivuyo ameishukuru TISEZA kwa kuanzisha kampeni hii yenye lengo la kuendelea kutoa elimu na kuwahamasisha watu wengi zaidi kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji Gambaless Timotheo amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanya uhamasishaji mkubwa wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.
Gambales amesema kuwa Watumishi Mara Amcos ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara iliitikia wito wa Serikali na kuandaa andiko ambalo lilipata ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.
“Kwa sasa Watumishi Mara Amcos inavizimba vinne na tayari imeshavuna samaki katika msimu wa kwanza na matarajio ni kuongeza vizimba zaidi kwa kushirikiana na taasisi za kifedha” amesema Timotheo.
Timotheo amesema changamoto kubwa wanayoipata katika mradi huo ni upatikanaji na gharama za chakula cha samaki na kuongeza kuwa kwa sasa chakula kinatoka nje ya nchi na gharama zake ni kubwa kwa kuwa zinaunganishwa na gharama za kusafirisha chakula na mawakala wa kuuza chakula hiyo kuwa ni wachache.
Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi wa mradi wa Rusaso General Supply Limited Charles Makoye amesema kampuni yao ina vizimba 25 kwa sasa na kati ya hiyo 18 vinasamaki na vingine havina samaki kwa sasa.
Makoye amesema soko la samaki lipo vizuri na kampuni yao na kwamba changamoto kubwa inayowakabili katika ufugaji wa samaki wa vizimba ni wadudu aina fish mali kufanya uhabifu wa kutoboa nyavu za samaki ikiwemo upatikanaji wa chakula cha samaki, uhaba na ubora wa vizimba.
“Kampuni yetu katika mpango wa baadaye inatarajia kuanzisha kiwanda cha chakula cha samaki ili kukabiliana na uhaba wa upatikanaji wa chakula cha samaki katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa” amesema Makoye.
Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani imeanza tarehe 18 Januari, 2026 hadi tarehe 09 Aprili, 2026 itaendeshwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na imeanza kutekelezwa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa na Kauli mbiu ”Unawezeshwa Kuwekeza kwa kupewa Unafuu wa Mtaji”.










