Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Akutana na Ujumbe Kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria

0


Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samwel M. Maneno, amekutana na kufanya kikao na Ujumbe kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), ukiongozwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Nchini Bw. George Mandepo.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.

Kikao hicho kimelenga kujadili namna bora ya kutekeleza maagizo na maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya kurekebisha Sheria kuhakikisha maboresho katika sheria nchini yanafanyika ili ziendane na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.

Vilevile, kikao hicho kimejadili utafiti wa kina na mapitio ya sheria zote zinazogusa maeneo ya kimkakati kama vile uwekezaji, biashara ya kidijitali, rasilimali watu, na nishati ili kuhakikisha zinatoa fursa kwa ukuaji wa uchumi wa kisasa.

Katika kikao hicho, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliambatana na Mkurugenzi Msadizi wa Makubaliano ya Kimataifa, Bw. Sunday Hyera, Wakili wa Serikali Mkuu, Dr. Shadrack Jaba, Mkurugenzi Msaidizi Urekebu, Bw. Chiki Chota kutoka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria na Wakili wa Serikali, Bw. Nyamhanga Nyamhanga.

Aidha, katika kikao hicho, wengine waliombatana  na Katibu Mtendaji wa Tume, ya Kurekebisha Sheria nchini, Bw. George Mandepo, ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Mapitio ya Sheria, Bw. Burhan Kishenyi, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Bi. Juliana Munisi, Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Sheria kwa Umma,  Bi. Zainab Chanzi, na Mkuu wa Sehemu ya Tathimini ya Sheria, Dkt. Annet Mnzava.

chanzo: ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top