Naibu Meya Manispaa ya Musoma Awataka Watumishi wa Serikali za Mitaa na Kata Kuimarisha Ulinzi

0


Naibu Meya  ambae ni Diwani wa kata ya Nyasho katika Manispaa ya Musoma Haji Mtete amewataka watumishi wa serikali  za Mitaa na kata, kusimamaia majukumu yao vizuri Kwa mujibu wa Sheria kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa katani humo.

Kauli hiyo ameitoa Leo kwenye kikao Cha WDC Cha robo ya pili ya mwaka 2025/2026kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kata hiyo uliopo ofisini hapo 

Mtete amesema  mipango ambayo inahitaji kufanyiwa kazi Kwa haraka yafanyiwe  haraka ili kutatua changamoto  Kwa lengo kupata mafanikio mazuri.

Kuhusu elimu amewataka walimu wakuu kuwapa taarifa wazazi  juu ya masuala ya  majukumu ya shule badala ya kuwaeleza watoto Kwa kuwa wao hawahusiki  na majukumu ya shule .

Aidha amewataka kuwashauri wazazi kuwafanyia vipimo vilivyo sahihi  watoto wao pindi wanapowapeleka watoto wao kuanzia kidato cha kwanza  ili kujua hali za afya zao kunusuru changamoto za afya shuleni  badala kutoa taarifa zisizo sahihi.

"Nendeni mkatoe elimu  juu ya suala hili la vipimo Kwa jamii na wazazi   Ili kusaidia watoto pindi wanapokuwa shuleni maana itasaidia kuelewa afya zao Kwa usahihi."amesema Naibu Meya Mtete.

Licha ya hilo,pia eneo la machinjio ya kuku  limeguswa kuwa sio eneo rafiki kimazingira  na kuwataka kuchukua hatua  za kisheria na kwamba wafanyabiashara kwenye maeneo ya maduka waweke dazibini za taka badala ya kutupa ovyo takataka.

Katika idara ya Kilimo,ufugaji na uvuvi,amemuagiza Afisa mifugo  kuchukua Sheria dhidi ya wafugaji wanahifadhi mifugo yao kutosababisha mgogoro  ya uharibifu wa mazao  kwa wakulima  .

Kwa upande wake  mtendaji wa kata hiyo RaymundMwambujule amewashauri watendaji wenzake  wa Mitaa kwenda kusimamaia vizuri vitendo viharifu vinavyofanywa Mitaa I badala ya kuwaachia venyeviti  na Askari Kwa kuwa serikali imewapa  dhamana hiyo .



Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top